TAFCA Mwanza yamkingia kifua Matola

CHAMA cha Makocha Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Mwanza kimeungana na baadhi ya mashabiki na wadau wa soka nchini wanaompigia chapuo kocha mzawa Selemani Matola kuaminiwa na Simba na kupewa jukumu la kukinoa kikosi hicho moja kwa moja. Matola amedumu Simba kama kocha msaidizi kwa takriban miaka 10 akiwa chini ya makocha wengi wa kigeni katika…

Read More

SMZ yaahidi kuimarisha sekta ya michezo Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema  itaendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha sekta ya michezo inaimarika zaidi na kutoa faida chanya kwa wanamichezo. Hayo yamesemwa leo Jumapili Desemba 7, 2025 na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla katika bonanza la mchezo wa mazoezi ya viungo, lililofanyika Kinduni, Kaskazini Unguja.  Hemed amesema, hayo…

Read More

Bao la Dube bado lamliza Kulandana

KIUNGO wa Fountain Gate, Abdallah Kulandana bado anaweweseka na kipigo cha mabao 2-0 ilichopewa timu hiyo na Yanga, huku akilitaja bao la Prince Dube lililotokana na penalti kuwa ndilo lililowatoa mchezoni na kujikuta wakipoteza mechi hiyo inayokuwa ya sita msimu huu. Kipigo hicho kilichopatikana kwenye Uwanja wa KMC kilikuwa cha pili mfululizo kwa timu hiyo…

Read More

Coastal v Yanga vita ipo hapa!

WAGOSI wa Kaya, Coastal Union usiku wa leo watakuwa wenyeji wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara, huku wakiwa na rekodi ya unyonge wa kupasuka mechi nane mfululizo mbele ya watetezi hao tangu 2022, jambo lililowafanya mabosi wa klabu hiyo kushtuka na kuapa leo ni leo. Coastal inaipokea Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini…

Read More

Kihongosi:  CCM msikae kimya, kemeeni upotoshwaji mtandaoni

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenan Kihongosi amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho, kutokuwa wanyonge bali kujibu mashambulizi ya upotoshwaji unaofanywa mtandaoni dhidi ya Serikali. Amewataka Wana CCM kujibu mapigo hayo, kwa kuwaelimisha Watanzania lakini si kwa kuwatukana watu hao wanaofanya uchochezi, upotoshaji na kubeza jitihada za kuleta…

Read More

Singida Black Stars v TRA United kazi ipo hapa!

BAADA ya vigogo vya soka Simba na Yanga kumaliza kazi juzi kwa ushindi nyumbani dhidi ya Fountain Gate na Mbeya City mtawalia, uhondo wa Ligi Kuu Bara unaendelea leo Jumamosi kwa mechi mbili za kibabe ikiwamo ya Singida Black Stars dhidi ya TRA United. Juzi Yanga iliikandika Fountain kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa KMC…

Read More

Azam ya Ibenge tatizo namba tu

ACHANA na rekodi iliyoandikwa na Azam FC kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kikosi hicho chini ya kocha mwenye uzoefu Afrika, Florent Ibenge kinapitia wakati mgumu kutokana na namba kukikataa. Ipo hivi. Azam inapitia nyakati ngumi kupata matokeo ya ushindi kwani mara ya mwisho furaha ya ushindi ni pale ilipofuzu hatua ya makundi…

Read More