
BDL KAZI IPO… Tausi Royals, Dar City hazitanii, Savio mmh!
LIGI ya Kikapu Dar es Salaam (BDL) inayoshirikisha timu za wanaume na wanawake, imezidi kushika hisia za wengi huku baadhi ya watu wakifungwa midomo baada ya kuona miamba miwili wa msimu uliopita Dar City na Tausi Royals msimu huu zitachemsha. Timu hizo zimeendeleza ubabe katika ligi hiyo zikionyesha wazi zilijiandaa kufanya makubwa tofauti na wengi…