Buzungu mbioni kurejea Mtibwa Sugar

KIUNGO wa Kagera Sugar, Omary Buzungu ameuomba uongozi wa timu hiyo umruhusu arejee Mtibwa Sugar baada ya kikosi cha ‘Wanankurukumbi’ kushuka daraja ikiwa ni miezi sita  tangu nyota huyo alipojiunga nacho wakati wa dirisha dogo la Januari, mwaka huu. Nyota huyo alijiunga na Kagera Sugar katika dirisha dogo la Januari 2025 akiwa ni pendekezo la…

Read More

Ngecha apigiwa hesabu Dodoma | Mwanaspoti

UONGOZI wa Dodoma Jiji uko katika mazungumzo kumrejesha beki wake wa kati wa zamani, Ibrahim Ngecha baada ya Vedastus Masinde wa TMA ya Arusha aliyehitajika mwanzoni kudaiwa anakaribia kujiunga na kikosi cha Simba. Masinde ni miongoni mwa mabeki waliohitajika na timu mbalimbali zikiwemo Singida Black na Dodoma Jiji, lakini inaelezwa yupo hatua za mwisho kwenda…

Read More

Bado Watatu – 16 | Mwanaspoti

“Sijambo. Karibu” Msichana akanijibu huku akinitazama kwa macho ya udadisi. “Sijui kama unanikumbuka?” “Nakukumbuka, ulikuja juzi kumuulizia mtu fulani , nikakwambia hatumfahamu” “Sasa nimekuja tena kwa tatizo hilo hilo. Nakumbuka uliniambia kwamba nyinyi ni wapangaji, sasa nilikuwa namhitaji mwenye nyumba hii” “Nakumbuka nilikwambia mwenye nyumba haishi hapa, anaishi Iringa” “Nipatie hata namba yake” “Anayo mume…

Read More

Straika Singida BS kubaki Pamba Jiji

BAADA ya mshambuliaji wa Singida Black Stars, Abdoulaye Yonta Camara, raia wa Guinea kukitumikia kikosi cha Pamba Jiji kwa mkopo wa miezi sita kwa msimu wa 2024-2025, mabosi wa timu hiyo wanafanya mazungumzo ya kuendelea kubaki naye. Camara alijiunga na Singida Agosti 14, 2024, ingawa sababu za kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara ziliwafanya…

Read More

Fadlu awatega mastaa Simba | Mwanaspoti

KOCHA wa Simba, Fadlu Davids mjanja sana baada ya kupata uhakika ukuta wa timu hiyo umeimarika zaidi kwa kutua beki wa kati mwingine mpya, Wilson Nangu na kipa wa Taifa Stars, Yakoub Suleiman ametoa kauli inayoonekana kama mtego kwa mastaa. Kocha huyo amesema anawasubiri wachezaji hao kambini waungane na timu ili ajue namna ya kuwatumia,…

Read More

Chikola ajishtukia mapema Yanga | Mwanaspoti

YANGA inaendelea kujifua kwenye kambi yao iliyopo Avic Town, Kigamboni chini ya kocha Romain Folz, lakini kuna winga mmoja mpya aliyetua klabuni hapo hivi karibuni amejishtukia baada ya kukiangalia kikosi hicho na fasta akaamua kujiongeza mwenyewe ili mambo yawe mepesi. Nyota huyo ni kiungo mshambuliaji aliyetua Jangwani kutoka Tabora United, Offen Chikola amesema kwa namna…

Read More

Salum Mwalimu aahidi Tanzania ya ‘maziwa na asali’

Tanga. Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu amewaomba Watanzania kumchagua kwa kishindo ifikapo Jumatano Oktoba 29, 2025, ili alitengeze taifa lenye ustawi na neema, akiahidi kuigeuza Tanzania kuwa “nchi ya maziwa na asali’ iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu. Akihutubia wakazi wa Muheza katika viwanja vya Madaba, jijini Tanga kwenye…

Read More

Gamondi: Kwa Aucho, Chama subirini muone

SINGIDA Black Stars leo usiku inaanza kampeni ya kusaka taji la kwanza msimu huu itakapovaana na Coffee ya Ethiopia katika michuano ya Kombe la Kagame, huku kocha mkuu Miguel Gamondi akiwataja mastaa watatu wa zamani wa Yanga. Gamondi amesema uwepo kwa Khalid Aucho, Clatous Chama na Nickson Kibabage utamsaidia katika mechi kubwa za ndani na…

Read More

Namungo, City FC Abuja hakuna mbabe

MCHEZO wa Kundi C katika michuano ya Tanzanite Pre-Season International baina ya Namungo ya Tanzania Bara na City FC Abuja kutoka Nigeria, umemalizika kwa sare ya bao 1-1. Mshambuliaji wa Namungo, Heritier Makambo alifunga bao la mapema dakika ya tatu kwa ustadi mkubwa kufuatia pasi ya Abdulaziz Shahame. Bao hilo liliwafanya wachezaji wa Namungo kucheza…

Read More