Watatu Simba wajiandaa kutua Yanga

SIMBA Queens imeshawapa taarifa wachezaji ambao haitakuwa nao msimu ujao na kati yao watatu wanahusishwa kujiunga na Yanga Princess. Wachezaji hao ni kiungo Ritticia Nabbosa, Asha Djafar na Precious Christopher ambao mikataba yao kikosini hapo imeisha. Asha Djafar aliyedumu kikosini hapo kwa misimu mitano mfululizo akiisaidia Simba kubeba mataji mbalimbali, amepewa taarifa hatakuwa sehemu ya…

Read More

JKT Queens yabeba kipa Mashujaa

JKT Queens msimu huu ndiyo itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya CECAFA ya kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa Wanawake na tayari imeanza maboresho kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo langoni. JKT itashiriki michuano hiyo baada ya kuwa mabingwa wa ligi msimu huu. Hii inakuwa mara ya pili kwa timu hiyo baada ya mwaka 2023 kuibuka mabingwa wa…

Read More

Nassor Kapama mbioni kutua Tabora United

KIUNGO mkabaji wa zamani wa Simba, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar, Nassor Kapama licha ya kushindwa kuibakisha timu yake anatajwa kujiunga na Tabora United kwa ajili ya msimu ujao 2025/26. Kapama ambaye alirejea Kagera Sugar akitokea Mtibwa Sugar amemaliza mkataba wake na waajiri wake hao hivyo ataondoka akiwa mchezaji huru. Chanzo cha kuaminika kutoka kwa…

Read More

Nickson Kibabage kumfuata Kijili Singida Black Stars

BEKI wa zamani wa Yanga, Nickson Kibabage ambaye amemaliza mkataba na timu hiyo aliyoitumikia kwa miaka miwili anatajwa kurejea kwa waajiri wake wa zamani Singida Black Stars iliyomnyakua beki wa kulia wa Simba, Kelvin Kijili. Kibabage alijiunga na Yanga kwa mkopo wa miezi sita na baadae kumnunua mazima kwa mkataba wa miaka miwili ambayo imetamatika…

Read More

Habari mpya kuhusu Kocha wa Yanga

YANGA inaendelea na marekebisho kadhaa ya kiufundi kwenye kikosi chake kuelekea kwenye maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa. Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo, inaripotiwa kwamba wataweka kambi ya maandalizi nchini Rwanda wiki chache zijazo. Lakini habari mpya ni kwamba jina la Kocha kijana Mfaransa mwenye…

Read More

Mecky Maxime atajwa Mtibwa Sugar

LICHA ya kuipambania Dodoma Jiji kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi msimu ujao 2025/26, Kocha Mecky Maxime hatakuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo akitajwa kurudi Mtibwa Sugar. Maxime alijiunga na Dodoma Jiji, Juni 19, 2024 akitokea Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars na anatajwa kurudi timu aliyoicheza na kuifundisha kwa muda…

Read More

Che Malone mlangoni Simba | Mwanaspoti

Licha ya Simba kushindwa kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo timu mbalimbali zinaendelea kupishana kuwania saini za baadhi ya nyota wa klabu hiyo ya Msimbazi. Che Malone, alitua Msimbazi misimu miwili iliyopita akitokea Coton Sport ya Cameroon na kutengeneza ukuta mgumu sambamba na Henock Inonga aliyetimka klabuni…

Read More

JKU Princess mabingwa Ligi ya Wanawake Zanzibar

KIKOSI cha JKU Princess, kimeibuka mabingwa wa Ligi Kuu Soka Wanawake Zanzibar (ZWPL) baada ya kuifunga Sauti Sisters mabao 2-0. Wakati JKU Princess ikiwa bingwa wa ligi hiyo iliyoshirikisha timu nne, Warriors Queens imemaliza ligi hiyo bila kuvuna pointi hata moja. Ligi hiyo imetamatika Alhamisi ya Julai 10, 2025 ulipochezwa mchezo huo ulioipa ubingwa JKU…

Read More

Beki mkongoman atajwa Azam FC

AZAM FC imeanza mazungumzo na Al Hilal ya Sudan ili kupata saini ya beki wa kulia, mkongomani Steven Ebuela, ambaye yuko nchini kwa takriban wiki sasa. Azam imeanza maandalizi mapema ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2025/26, ikiwatambulisha baadhi ya wachezaji wake akiwemo kipa Aishi Manula, Muhsin Malima, Lameck Lawi na Kocha Florent Ibenge….

Read More