
Manyika aingia Namungo na mkakati wa kufuta rekodi mbovu ya kuruhusu mabao mengi
Rekodi ya Namungo kuwa na wastani wa kuruhusu mabao 30+ katika kila msimu ndani ya misimu sita iliyoshiriki Ligi Kuu Bara tangu 2019-2020, imemfanya kocha wa makipa wa kikosi hicho, Peter Manyika, kuingia na mpango kazi maalum. Manyika amesema katika kuhakikisha lango la timu hiyo linakuwa salama zaidi, anapambana kuwaandaa vijana wake kuwa katika kiwango…