Kijo kocha mpya Zanzibar Sand Heroes

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), limemteua Kijo Nadir Nyoni kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Soka la Ufukweni. Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Juni 27, 2025 na Ofisa Habari wa ZFF, Mohamed Kabwanga, imesema kocha huyo ana diploma C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika(CAF) na alishawahi kupata mafunzo…

Read More

Hersi, Arafat, Ibwe wajitosa CCM kuwania ubunge

RAIS wa Yanga, Hersi Said, Makamu wake Arafat Haji na Ofisa Habari na Mawasiliano msaidizi wa Azam FC, Hasheem Ibwe, leo Juni 28, wamejitosa  kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyia Oktoba, mwaka huu. Hersi amechukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Kigamboni jijini…

Read More

Aziz KI amtaja Pacome Marekani

WAKATI timu anayoichezea sasa ya Wydad Casablanca ya Morocco ikiaga fainali za Kombe la Dunia la Klabu, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki amevunja ukimya akazungumza na Mwanaspoti kutokea Marekani. Unaambiwa kwamba mchezaji huyo ambaye aliondoka Yanga akiwa na faida nyingi ikiwamo kumuoa binti mrembo wa Kitanzania, mwanamitindo Hamisa Mobetto, kaiambia Mwanaspoti kwamba kuna jambo ambalo…

Read More

Hamdi ashtukia jambo Yanga mapema

KUCHEZA mechi nne za mashindano ndani ya kipindi cha takribani siku 11, imeonekana kuwa ni changamoto kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi. Hata hivyo, kocha huyo amesema anapambana na hali hiyo kwani hana namna ya kufanya zaidi ya kuzicheza mechi hizo na kufanikisha malengo. Hamdi ameyasema hayo kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la…

Read More

Ouma ataja mambo matatu akiikabili Yanga

KOCHA wa Singida Black Stars, David Ouma amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo wa fainali huku akitaja mambo matatu waliyojiandaa nayo. Singida Black Stars kesho Juni 29, 2025 itacheza dhidi ya Yanga katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) utakaofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku. Timu hizo…

Read More

Asante Kotoko yaitibulia Yanga Afrika Kusini

Kama Yanga ilikuwa na mpango wa kutetea ubingwa wa Kombe la Toyota mwaka huu huko Afrika Kusini, umekufa rasmi baada ya waandaaji wa mashindano hayo kuialika timu ya Asante Kotoko ya Ghana. Timu hiyo ya Ghana ndio itacheza kama mwalikwa katika mechi hiyo ambayo huwa dhidi ya wenyeji Kaizer Chiefs na sio Yanga ambayo ndio…

Read More

Simba yatua Ivory Coast kusaka mbadala wa Camara

MABOSI wa Simba wameanza kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu ujao ili kuongeza ushindani, huku suala la makipa likiwa kitendawili kutokana na kuripotiwa kutaka kuachana na Moussa Camara, jambo ambalo limewapeleka hadi Mauritania kupambana kunasa saini moja matata. Camara aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Horoya AC ya kwao Guinea, inaelezwa huenda akaachana na…

Read More

Umemzingatia pilato Amin Omar? | Mwanaspoti

MCHEZO wa Dabi ya Kariakoo umemalizika ukihitimisha msimu wa Ligi Kuu Bara 2024-2025 na kutoa jibu la bingwa baada ya Yanga kuichapa Simba mabao 2-0, ushindi ambao umeifanya timu hiyo kutwaa ubingwa huo mara nne mfululizo na 31 kihistoria. Mchezo huo umeiingiza Tanzania kwenye historia mpya baada ya kuamuliwa na waamuzi kutoka Misri. …

Read More