Mgaza miwili tena Dodoma Jiji

MABOSI wa Dodoma Jiji, wamemalizana na mshambuliaji wao, Yassin Mgaza kwa kumuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi msimu wa 2026-2027. Mshambuliaji huyo alijiunga na Dodoma jiji Julai 2023 akitokea KMKM ya Zanzibar, ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili ambao umefikia ukingoni msimu huu. Umuhimu wake kikosini hapo umempa ulaji mpya. Chanzo cha kuaminika…

Read More

Camara atibuliwa Simba | Mwanaspoti

KITENDO cha kipa wa Simba, Moussa Camara kuruhusu mabao mawili katika mechi ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, kimemfanya nyota huyo kushindwa kuandika rekodi mpya ya kumaliza msimu akiwa na ‘clean sheets’ nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu Bara. Camara aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Horoya AC ya kwao Guinea, amemaliza ligi akiwa kinara…

Read More

Rekodi ya Mkude yaendelea kuishi

LICHA ya kiungo wa Yanga, Jonas Mkude kutocheza mechi ya juzi ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba, ila nyota huyo ameendeleza rekodi nyingine bora ya kutopoteza mechi yoyote ya dabi hiyo kwenye Ligi Kuu Bara, akiwa amechezea timu hizo zote mbili. Katika mechi hiyo ya juzi, Yanga ilishinda mabao 2-0, yaliyofungwa na Pacome Zouzoua…

Read More

Dabi yampa Oumba mbinu za ushindi fainali FA

DAKIKA 90 za mchezo kati ya wenyeji Yanga dhidi ya watani zao Simba zimemtosha kocha wa Singida Black Stars, David Ouma kutambua ni wapi anatakiwa kufanyia kazi kabla ya kuvaana na timu hiyo Jumapili hii na kushinda. Ouma ameliambia Mwanaspoti alikuwa na dakika 90 za kuisoma Yanga ikiifunga Simba kwa mabao 2-0 huku akibaini ubora…

Read More

Ubingwa wa Yanga wamuibua Ramovic

BAADA ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya nne mfululizo, aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Sead Ramovic amevunja ukimya na kutoa pongezi kwa klabu hiyo, huku akieleza fahari yake kwa kuwa sehemu ya mafanikio hayo. Ramovic, ambaye aliiongoza Yanga katika mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2024/25 kabla ya kutimkia…

Read More

Dube ashindwa kujizuia, achekelea taji Ligi Kuu Bara

KWA miaka minne alicheza katika Ligi Kuu Bara akiwa na Azam FC. Msimu baada ya msimu, ndoto yake ya kutwaa ubingwa iliendelea kuwa mbali licha ya juhudi kubwa alizoweka uwanjani.  Lakini msimu huu wa 2024/25, hatimaye Prince Dube, mshambuliaji kutoka Zimbabwe, amevuna alichokipanda akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi kwa kishindo….

Read More

Kilichowaponza JKT, UDSM DBL ni hiki hapa

Kujiamini kwa JKT na UDSM Outsiders,  ndiko kulikofanya hadi timu hizo zikapoteza michezo yao miwili ya Ligi ya  Mkoa wa Dar es Salaam (BDL). Ligi hiyo ambayo kwa sasa imesimama kupisha mashindano ya Kombe la Taifa, imekuwa na ushindani mkubwa tofauti  na miaka iliyopita. JKT iliyokuwa ikijiamini itashinda, ilifungwa na UDSM iliyoondokewa na nyota wake…

Read More

Straika JKT Tanzania kiroho safi

MSHAMBULIAJI wa JKT Tanzania, Edward Songo amesema msimu wa Ligi Kuu Bara uliomalizika jana Jumatano ulikuwa  mzuri kwao, lakini umewaachia somo la kujipanga ili ujao wa 2025/26 waweze kufanya makubwa zaidi. Songo ambaye amemaliza msimu akiwa na mabao sita na asisti mbili, alisema kitendo cha timu hiyo kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi…

Read More

Hoza apewa miwili Dodoma Jiji

KIUNGO mkabaji wa Dodoma Jiji, Salmin Hoza ataendelea kusalia kwenye klabu hiyo hadi 2027 baada ya kuongeza mkataba miaka miwili. Kiungo huyo alijiunga na Dodoma Jiji 2020 kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Azam FC hadi sasa ameendelea kuitumikia timu hiyo akiwa mchezaji halali wa klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba na waajiri wake wa…

Read More