TFF na Bodi waitwa mahakamani Dar

KUNA kitu kinaendelea Mahakamani kikilihusu Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF) na Bodi yake ya Wadhamini. Na wito wa kuitwa Mahakamani umetolewa leo Jumatatu, Juni 16,2025 na Jaji Butamo Phillip anayesikiliza shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam. Iko hivi; TFF, kupitia…

Read More

Mastaa Tabora United wana jambo lao

WAKATI kikosi cha Tabora United kikijiandaa na mechi ya keshokutwa Jumatano ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, wachezaji wa timu hiyo wanadaiwa kuweka mgomo baridi hadi pale ambapo watakapolipwa mishahara ya miezi miwili. Timu hiyo imebakisha mechi mbili za kuhitimisha msimu huu ikianza ugenini kesho dhidi ya Azam, huku kikosi hicho cha Nyuki…

Read More

Yanga yapaa kwenda Mbeya, yawaacha wawili Dar

KIKOSI cha Yanga kimeondoka jioni hii kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya tayari kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons huku ikiwabakiza mjini wachezaji wawili tu miongoni mwa nyota wa kikosi hicho kinachonolewa na kocha Miloud Hamdi. Yanga itavaana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini humo keshokutwa Jumatano ikiwa ni…

Read More

Ligi ya Kikapu Dar mambo ni moto

MECHI saba za mwisho kabla Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ( BDL) kusimama kupisha michuano ya Taifa Cup, timu zilionyesha ushindani mkali uliyowapa mashabiki burudani katika viwanja vya Don Bosco vilivyopo Upanga, Dar es Salaam. Kwa sasa ligi hiyo imesimama ili kutoa nafasi ya kujiandaa kwa timu za mikoa zinazokwenda kushiriki michuano…

Read More

Wapiga mbizi waikuna BMT | Mwanaspoti

OFISA Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Charles Maguzu, ameupongeza uongozi Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA) kutumia mashindano kuimarisha ukanda wa CECAFA na kuvitaka vyama vingine vya michezo hapa nchini kuwa na utaratibu wa kualika timu za nchi jirani katika mashindano yao. Maguza ameyasema hayo jana Jumapili alipokuwa anafunga msimu wa mashindano kwa…

Read More

Marefa wa ngumi kupigwa msasa

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imesema itaendelea kutoa kozi ya waamuzi wa mchezo ili kuongeza weledi katika kazi zao. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa TPBRC, Emmanuel Saleh alipokuwa anafunga kozi ya mafunzo kwa waamuzi yaliyofanyika jana Fit Poa Gym iliyopo Masaki, Dar es Salaam. Saleh amesema lengo la mafunzo hayo ni…

Read More

Coastal Union waitana Tanga | Mwanaspoti

WAGOSI wa Kaya ‘Coastal Union’ wanajiandaa kuzipokea timu za Fountain Gate na Tabora United katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara za kufungia msimu huu, lakini mabosi wa klabu hiyo wamewaita wanachama ili kujadili mipango kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025-2026. Uongozi huo umeitisha mkutano mkuu maalumu utakaofanyika Julai 12 kujadili taarifa ya maendeleo…

Read More

Fountain Gate yagoma kushuka daraja Bara

MKURUGENZI wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau, amesema mechi mbili zilizobaki zinaipa nafasi timu hiyo kutokushuka daraja kutoka Ligi Kuu. Aidha, Makau amesema timu yake ya vijana umri chini ya miaka 20 ilistahili kuwa bingwa, huku akitaja bao la ushindi la Azam FC lilikuwa ni la utata. Makau aliyasema hayo hayo mchana huu, baada ya…

Read More