
Mtibwa Sugar yampigia hesabu Baleke
BAADA ya Mtibwa Sugar kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka msimu uliopita, mabosi wa timu hiyo wako katika mchakato wa kuboresha kikosi hicho, huku wakiwa wanampigia hesabu aliyekuwa mshambuliaji wa Simba na Yanga, Mkongomani Jean Baleke. Taarifa kutoka katika kambi ya kikosi hicho, zimeliambia Mwanaspoti, Baleke ambaye kwa sasa hana timu tangu alipoachana na Yanga…