Yanga yatuma salamu Msimbazi ikiichapa JKT Tanzania 5-0

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameendelea kuthibitisha ubora wao katika ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa nane mfululizo kufuatia kuwachapa Maafande wa JKT Tanzania mabao 5-0, mechi iliyopigwa leo Jumatano Februari 25, 2026 kwenye Uwanja wa KMC, Dar. Ushindi huo mnono unaifanya Yanga kama kutuma salamu kuelekea kwenye Dabi ya Kariakoo…

Read More

Julio ashtuka, aomba mechi za kirafiki

JAMHURI Kihwelo ‘Julio’ baada ya kuiongoza Mashujaa katika mechi mbili akiwa kocha mkuu akishinda zote ikiwamo dhidi ya Mtibwa Sugar Ligi Kuu na ile ya Kombe la Shirikisho mbele ya Nkim, ameshtuka kisha kuomba mechi za kirafiki, huku akitoa sababu. Kocha huyo aliyechukua mikoba ya Salum Mayanga hivi karibuni, ameliambia Mwanaspoti kuwa, ameichungulia ratiba ya…

Read More

Neno la Cabaye akiuguza goti

KIUNGO wa Tanzania Prisons, Abdallah Masoud ‘Cabaye’ ambaye kwa sasa yupo nje ya uwanja akiuguza jeraha la goti ameweka wazi kuwa bado ana matumaini makubwa ya kurejea mapema kuisaidia timu hiyo kupambana na hatari ya kushuka daraja. Cabaye alipata jeraha hilo Novemba 26, 2025 wakati Tanzania Prisons ilipokubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Fountain…

Read More

Mayele afufuka baada ya siku 122

MSHAMBULIAJI wa Pyramids FC na timu ya taifa ya DR Congo, Fiston Mayele amemaliza ukame wa siku 122 baada ya juzi kufunga bao la Ligi Kuu ya Misri katika mechi ya ushindi wa mabao 3-1 wa timu hiyo dhidi ya Ghazl El Mahallah. Mara ya mwisho kwa nyota huyo wa zamani wa Yanga kufunga katika…

Read More

Prisons yaachana na Otieno, Nsajigwa atajwa kumrithi

BAADA ya Tanzania Prisons kufikia makubaliano ya pande mbili kuachana na Kocha Zedeckia Evans Otieno, inaelezwa iko katika hatua nzuri ya mikoba yake kumkabidhi Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ kutoka kwa maafande wa Transit Camp. Taarifa ya Tanzania Prisons kuachana na Otieno iliyotolewa leo Februari 25, 2026 na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, ‎Godfrey Madegwa, imesema:…

Read More

Mama lishe aliyegeukia udereva wa daladala

Dar es Salaam. “Asante, rubani wetu! Asante, mwanamke wa shoka, kwa kutufikisha salama salmini! Mungu akubariki sana!” Haya ni baadhi ya maneno yanayosikika kutoka kwa abiria wakimpongeza Joyce Foya kila anapowafikisha salama mwisho wa safari zao. Kauli hizo si za kawaida katika usafiri wa daladala, jijini Dar es Salaam, bali ni ishara ya heshima na…

Read More