Simba waache ubinafsi kwenye hili

KLABU za Barcelona na Real Madrid zina upinzani wa hali ya juu uwanjani na wakati fulani wachezaji huonekana kama wana chuki dhidi ya timu moja, kiasi kwamba baadhi ya mechi kati ya vigogo hao wa soka Hispania hutawaliwa na minyukano sehemu tofauti za uwanja. Picha za marudio ya baadhi ya mechi huonyesha jinsi mshambuliaji gwiji…

Read More

Sura mbili mpya zaonekana mazoezini Simba

KATIKA mazoezi ya Simba ambayo timu hiyo inaendelea kujiandaa na michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara iliyosalia, kuna sura mbili za wachezaji wapya wakijifua. Achana na kiungo mzawa Morice Abraham (22) ambaye alikuwa na kikosi hicho akifanya mazoezi tangu Aprili mwaka huu, kuna nyota wengine wapya wawili. Abraham ambaye alikuwa akiitumikia FK Spartak Subotica ya…

Read More

Mustafa apishana na Manula Azam FC

BAADA ya Azam FC kumalizana na aliyekuwa kipa wa Simba, Aishi Manula mabosi wa klabu hiyo kwa sasa wapo hatua za mwisho kuvunja mkataba wa mwaka mmoja na Mohamed Mustafa. Mustafa raia wa Sudan, alisajiliwa na Azam kutoka El Merrikh ya Sudan baada ya mkataba wa awali wa mkopo kumalizika ikimsajili kwa mkataba wa miaka…

Read More

Yanga, TFF hakijaeleweka | Mwanaspoti

SAKATA linaloendelea kati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Yanga kuhusu madai ya fedha za ubingwa wa Kombe la Shirikisho (FA), limechukua sura mpya baada ya kutofikia kwa maelewano. Hivi karibuni kumekuwa na mzozo unaoendelea kuhusiana na taasisi hizo mbili kwa kile kilichoibuliwa na Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe kuweka wazi hawatocheza mechi…

Read More

Injili ya Fyatu kwa mafyatu na maajabu ya Kaya

Katika kufanya utafiti wangu usio rasmi, nimegundua mambo ya ajabu. Naweza kujiita mgunduzi wa karne hii kwenye sayansi ya jamii. Nianze na niliyogundua. Mosi, nimegundua kuwa fyatu anaweza kwenda shule asielimike. Kifyatu, hii inaitwa education for ignorance. Fyatu anaweza kuoga lakini akabaki mchafu achia mbali kutakata. Pili, Fyatu anaweza kula kwa miguu na mikono lakini…

Read More

Majimbo haya Singida usibeti, kila mtu bingwa

Singida. Ni kama watu wanaoisubiri ile siku ya kuja Masihi! ndivyo ilivyo kwa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wenye nia ya kugombea ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Singida huku kila mmoja akiota kwamba kuna mtu ‘amekanyaga waya’ ili siku zisitembee. Hiyo inajidhihirisha kwa namna joto lilivyopanda huku makada wakianza kujipitisha kwenye mikusanyiko na…

Read More

Nyota Savio aongoza kutupia BDL

WAKATI ushindani wa ufungaji ukiendelea katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), huko kunaonyesha kwamba  nyota wa Savio, Ntibomela Bukenge ndiye anayeongoza kwa ufungaji akiwa keshatupia pointi 124. Mchezaji huyo amegeuka moto katika mashindano hayo na ubora wake umekuwa ukionekana kila anapokuwa karibu na nyavu, kwani ni nadra kukosa kikapu anaposhuti. Bukenge…

Read More

Zamalek washusha mzigo Yanga | Mwanaspoti

NDANI ya wiki chache zijazo, mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ataweka rekodi mbili kwenye soka la Tanzania endapo dili lake la kucheza nje litakwenda kama lilivyopangwa. Rekodi ya kwanza ni kwamba anakwenda mchezaji wa kwanza wa Tanzania Bara kuuzwa kwa dau kubwa zaidi nje ya nchi, lakini pili anakuwa staa wa kwanza mzawa kununuliwa na…

Read More