
Injili ya Fyatu kwa mafyatu na maajabu ya Kaya
Katika kufanya utafiti wangu usio rasmi, nimegundua mambo ya ajabu. Naweza kujiita mgunduzi wa karne hii kwenye sayansi ya jamii. Nianze na niliyogundua. Mosi, nimegundua kuwa fyatu anaweza kwenda shule asielimike. Kifyatu, hii inaitwa education for ignorance. Fyatu anaweza kuoga lakini akabaki mchafu achia mbali kutakata. Pili, Fyatu anaweza kula kwa miguu na mikono lakini…