Sakata la Dabi, Ally Kamwe aibua mambo mapya

MSEMAJI wa Yanga,  Ally Kamwe amesema klabu hiyo, iko siriazi katika msimamo wa kutocheza mechi ya Kariakoo Dabi dhidi ya Simba, akisema Bodi ya Ligi Tanzania imepotosha juu ya matakwa yao manne. Akizungumza jioni hii katika makao makuu ya Yanga, Kamwe amesema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo ameshindwa kufafanua vizuri matakwa manne kwamba…

Read More

TFF: Hakuna atakayesajiliwa bila kupima moyo

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema msimu wa 2025/26 hakuna mchezaji ambaye atasajiliwa kucheza Ligi Kuu Bara au Ligi ya Championship bila kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo. Karia ameyasema hayo leo Juni 9, 2025 baada ya TFF na Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania kuingia makubaliano na Taasisi ya Moyo…

Read More

Mpole ashtuka, aanza kujifua mapema

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Geita Gold, FC Lupopo ya DR Congo na Pamba Jiji, George Mpole, aliye nje ya uwanja tangu dirisha dogo la usajili lilipofungwa Januari mwaka huu, ameshtuka na kuanza kujifua mapema akijiandaa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara. Mfungaji Bora huyo wa Ligi Kuu msimu wa 2021-2022, amesema licha ya kukaa…

Read More

Karia: Mchezaji bila kupimwa moyo hakuna kucheza Ligi

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema msimu wa 2025/26 hakuna mchezaji ambaye atasajiliwa bila ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo kwa wachezaji wote wa Ligi Kuu na Ligi ya Championship. Karia ameyasema hayo baada ya TFF  pamoja na Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania (TMSA) kuingia makubaliano rasmi na Taasisi…

Read More

Bodi ya Ligi: Kariakoo Dabi ipo palepale

BODI ya Ligi Tanzania TPLB imesema katika mkutano wao na Yanga, klabu hiyo imekuja na mambo manne ambayo inataka yafanyiwe kazi kabla ya mchezo dhidi ya Simba. Akitangaza hayo mchana huu Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo amesema bodi yao imeyapokea na kwenda kuyafanyia kazi huku akisisitiza kwamba mchezo huo wa Juni 15, 2025…

Read More

Kisa Mbeya City, Prisons yajipanga upyaa

KUREJEA tena kwa Mbeya City katika Ligi Kuu Bara, kumeizindua Tanzania Prisons kuanza mipango mapema ya kujipanga ikitaka kusajili kikosi imara kitakachotengeneza ushindani wa kuwania nafasi za juu katika msimamo na sio kujikwamua kushuka daraja, kama ilivyopitia katika misimu ya hivi karibuni. Chanzo cha ndani kutoka timu hiyo, kilisema uongozi umeanza na kuweka skauti  kila…

Read More

Tanzania kuanza na Sudan Cecafa Dar

MASHINDANO ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ya Wanawake yanatarajiwa kuanza Juni 12, mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex ambapo Tanzania itaumana na Sudan Kusini. Timu tano kutoka ukanda wa Cecafa zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Junie 21 yakijumuisha Burundi, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania na bingwa mtetezi, Uganda. Mkurugenzi…

Read More

Viongozi Yanga watua Bodi ya Ligi na wanasheria

Yanga imefika rasmi katika kikao chao na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), huku msafara wa timu hiyo ukiwahusisha viongozi watano na wanasheria watatu. Msafara wa Yanga umefika saa 4:12 asubuhi ikiongozwa na Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai, Rodgers Gumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano….

Read More

Vigogo waanza kuwasili Bodi ya Ligi kujadili dabi

Mkutano wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na viongozi wa Yanga umeanza kuwakusanya vigogo mbalimbali wakianza kuwasili eneo la tukio. Mkutano huo unaofanyika asubuhi hii kwenye ofisi za TPLB zilizopo Ilala, jijini Dar es Salaam ambapo viongozi wameanza kufika wakitanguliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Almas Kasongo aliyefika saa 2:37 asubuhi. Baada ya…

Read More