Mtoto wa Mjini – 6
HUKU akiendelea kuwatazama kwa zamu vijana wale kutaka kuwakumbuka kama aliwahi kuwaona mahali, mzee Mangushi alijibu: “Marhaba…”Na baada ya kutambua sura zao zilikuwa ngeni machoni pake, akawauliza: “Niwasaidie nini?” “Kuna shida kidogo mzee wangu,” alisema mmoja wao na kumfanya mzee Mangushi kuutoa mwili wake wote nje ya mlango.“Shida gani tena?” alihoji uso wake ukitaliwa na wasiwasi.“Mimi…