Hili hapa Chama la Baum Ujerumani

WIKI zilizopita RB Leipzing ilimtambulisha kiungo Lisa Baum ambaye ana asili ya nchi mbili Tanzania na Ujerumani. Baum ambaye mara kadhaa aliwahi kusema anatamani kuitumikia timu ya taifa ‘Twiga Stars’ alijiunga na chama hilo akitokea Hamburger SV ya Ujerumani. Katika misimu miwili aliyoitumikia Hamburger SV ya Ligi daraja la kwanza alifunga mabao 10 kwenye mechi…

Read More

Pak Stars, Gymkhana zafunika daraja la tatu

KUPUNGUA kwa mvua jijini Dar es Salaam kumeamsha tena moto wa kriketi ambao umezileta ligi tatu tofauti katika viwanja vya Gymkhana, Leaders Club na Anadil Burhan, Ligi ya TCA-Diwa kwa wanaume, Ligi ya kufuzu michuano ya Caravans na Ligi B ya TCA kwa wanaume ndizo zilizoipamba kriketi mwishoni mwa juma. Timu zilizotoka kifua mbele ni…

Read More

Clara awavuruga mabosi Al Nassr

MOTO wa mshambuliaji wa Kitanzania, Clara Luvanga unazidi kuwachanganya viongozi wa Al Nassr ya Saudia na inaelezwa wako kwenye mchakato wa kumboreshea mkataba wake uliosalia mwaka mmoja. Kwa sasa nyota huyo mwenye makombe mawili ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudia yuko nchini kwenye majukumu ya timu ya taifa, Twiga Stars ambayo iko Dar es Salaam…

Read More

Dar Sprint yamtega tena Birdi Tanganyika Packers

BAADA ya kushinda mashindano matatu mfululuzo ya mbio za magari hadi nusu ya mwaka huu, Manveer Birdi atakuwa na mtihani mwingine mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Tanganyika Packers kuthibitisha ubora wake nyuma ya usukani. Toyota Dar Sprint, mbio fupi za mzunguko, ndiyo mtihani ambao Birdi anatakiwa kuushinda na kuudhihirisha umma kuwa yeye ndiye mbabe…

Read More

Beki KMC mambo bado Al Hilal

BEKI wa pembeni wa KMC, Raheem Shomary aliyeripotiwa kupewa ruksa ya kwenda kujiunga na Al Hilal ya Sudan, amekiri mambo bado, kwani hakijaeleweka, ila anajipa moyo muda si mrefu kila kitu kitakaa sawa. Nyota huyo aliyeibuka Mchezaji Bora Chipukizi kwa msimu wa 2023-2024, alikuwa katika hatua za mwisho kumalizana na Al Hilal ya Sudan, lakini…

Read More

Mgunda afichua kilichomtoa AS Vita

BAADA  kimya cha muda mrefu cha mshambuliaji Ismail Mgunda, hatimaye ameelezea sababu ya kuachana na AS Vita ya DR Congo aliyokuwa imemsajili akitokea Mashujaa inayocheza Ligi Kuu Bara. Mgunda wakati yupo Mashujaa alifunga mabao mawili na asisti nne, aliliambia Mwanaspoti juu ya safari nzima ilivyokuwa hadi kutemana na AS Vita ndani ya muda mfupi kwani…

Read More

Faili la Jonathan Sowah latua kwa MO

KABLA hata dirisha la usajili halijatangazwa kufunguliwa, mabosi wa klabu kubwa za soka nchini wameanza kazi kimyakimya kusaka nyota wapya kwa msimu ujao, huku faili ya straika wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah likitua kwa bilionea wa Simba, Mohammed ‘MO’ Dewji. Nyota huyo wa kimataifa kutoka Ghana, awali amekuwa akihusishwa na Yanga iliyoelezwa ilijifungia naye…

Read More

Dili la Diarra kutimka Yanga lipo hivi!

PENGINE taarifa hii itawashusha presha mashabiki wa Yanga, wanaoianza wiki ya kwanza ndani ya Juni, baada ya kubainika kuwa, lile dili la kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra anayetakiwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini limeota mbawa baada ya kuondolewa rasmi katika hesabu za mabosi. Iko hivi. Kaizer Chiefs ilikuwa na hesabu za…

Read More

Hamisa Mobetto ndani ya uzi wa Wydad

SIKU chache tangu, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayekipiga Wydad Casablanca ya Morocco, Stephane Aziz KI, mkewe ambaye ni  mrembo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto ametupia picha kadhaa akiwa ametinga uzi wa klabu hiyo ya Morocco. Hamisa alikuwa uwanjani jana wakati Wydad ikivaana na FC Porto, ambapo Aziz Ki kuingia uwanjani kwa mara ya kwanza…

Read More

Vyombo vya habari vyahimizwa kuzingatia usawa wa kijinsia

Dar es Salaam. Vyombo vya habari nchini Tanzania vimetakiwa kuzingatia usawa wa kijinsia kuanzia uratibu wa ndani ya vyombo hivyo hadi uripotiji wa habari zake. Imeelezwa usawa unaanzia kwa wafanyakazi, habari zisizogandamiza jinsia sambamba na kusimamia vyema sera za jinsia za vyombo hivyo. Wito huo umetolewa na Profesa Nancy Booker, Dean wa Shule ya wahitimu…

Read More