
Singida BS yapoteza tena dhidi ya Simba, vita bado mbichi
MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Uganda, Steven Mukwala, ameendelea kuonyesha thamani yake ndani ya Simba SC kwa kufunga bao pekee lililoiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars. Hiyo ilikuwa katika mechi ya kiporo ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa leo Mei 28, 2025 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini…