Laizer atwishwa zigo Fountain Gate
KOCHA mpya wa Fountain Gate, Mohamed Ismail ‘Laizer’, amefikia makubaliano ya kukiongoza kikosi hicho katika mechi mbili zilizobakia msimu huu, huku akiweka wazi sharti kubwa alilopewa ni kuhakikisha timu hiyo inabakia Ligi Kuu msimu ujao. Akizungumza na Mwanaspoti, Laizer alisema hahofii masharti aliyopewa kutokana na kuamini timu hiyo inaweza kujinasua katika janga la kushuka daraja,…