Imekuwa Jumapili ngumu kwa Simba 

LICHA ya wenyewe kujinasibu kwamba Jumapili huwa ni siku nzuri kwa klabu yao, lakini hali kwa Jumapili ya leo imekuwa kinyumw kwa Simba baada ya awali kuvurugana katika Mkutano Mkuu wa mwaka mapema asubuhi na usiku huu imekumbana na kipigo cha pili ikiwa ugenini huko Mali. Asubuhi Simba ilifanya mkutano ambao ulimalizika kitatanishi baada ya…

Read More

Meneja wa Yusuph Athuman afichua jambo

MENEJA wa Yusuph Athuman anayekipiga Napsa Stars inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia, Hon Simbeye amesema kama mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga ataendelea kupata nafasi ya kucheza huu unaweza kuwa msimu wake bora. Kabla ya kutimkia Zambia msimu uliopita alisajiliwa na Yangon United inayoshiriki Ligi Kuu Myanmar kabla ya kurejea Tanzania na kumaliza mkataba wake…

Read More

Takwimu za mbwana Samatta Le Havre

INGAWA nahodha wa timu ya taifa Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta hajafunga bao lolote akiwa na kikosi cha Le Havre ya Ufaransa katika dakika 518, takwimu zinaonyesha ni mchezaji hatari anapokuwa ndani ya boksi. Samatta alijiunga na Le Havre Agosti 05 mwaka huu akitokea PAOK inayoshiriki Ligi Kuu ya Ugiriki alipoitumikia misimu miwili akiipa ubingwa…

Read More

Aisha Masaka kumfuata Opah Hispania

MABOSI wa Brighton & Hove Albion wanaangalia uwezekano wa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Kitanzania, Aisha Masaka kwenda Hispania baada ya kutopata nafasi ya kucheza kikosini hapo. Mwanaspoti inafahamu mshambuliaji huyo wa timu ya taifa, Twiga Stars amebakiza mkataba wa mwaka mmoja England kati ya miwili na utamalizika mwishoni mwa msimu huu. Kiongozi mmoja anayemsimamia…

Read More

Sababu ya Suzana Adama kurejea Bongo

MENEJA wa mchezaji Suzana Adam, James Mlaga amesema sababu za kiungo huyo kurejea Bongo na kujiunga na Tausi FC inayoshiriki Ligi ya Wanawake ni kumjengea hali ya kujiamini baada ya kukaa nje kwa msimu mzima. Suzana msimu uliopita aliitumikia FC Masar ya Misri alikodumu kwa misimu miwili tangu alipojiunga nayo msimu wa 2022/23 akitokea Fountain…

Read More

Mkutano Simba waacha maswali kibao, Mangungu atakiwa kujiuzulu

MKUTANO Mkuu wa Simba wa mwaka 2025, umeisha saa 5:59 asubuhi, huku ukiibua maswali kwa wanachama kutokana na aina ya ulivyomalizika. Mkutano huo ambao awali ulihudhuriwa na wanachama 720, kisha baadae kuongezeka hadi 998, umemalizika huku wanachama hao wakiwa hawajui mustakabali wa yale yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho. Hatua hiyo, imejiri baada ya mapendekezo ya mabadiliko ya…

Read More

Simba inazitaka Sh 29 Bilioni msimu huu

SIMBA imetangaza kuwa, inakusudia kukusanya kiasi cha Sh 29.5 Bilioni kwenye msimu huu wa 2025/26 kama bajeti ya klabu hiyo. Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 13.5 kutoka bajeti ya mwaka uliopita ambayo ilikuwa ni kiasi Sh 26 Bilioni ikifanikiwa kukusanya Sh 24 Bilioni pekee ikipungukiwa sh 1.4 Bilioni. “Kuna mambo yalitukwamisha tukashindwa kufika kwenye…

Read More

Mkutano Mkuu Simba tafrani tupu

WAKATI Mkutano Mkuu wa mwaka wa Simba ukiendelea leo Kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, wanachama wa klabu hiyo wameonekana wakiwa katika hali ya tafrani huku baadhi ya ajenda zikiendelea kusomwa ukumbini hapo. Mkutano huo ambao umeitishwa kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya katiba ya Simba ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho…

Read More