
Baada ya Vijana kuifinya Savio UDSM, Stein kazi ipo
KIWANGO cha chini kilichoonyeshwa na Savio kilisababisha ifungwe na Vijana ‘City Bulls’ kwa pointi 70-50, katika Ligi ya kikapu Dar es Salaam inayofanyika katika Uwanja wa Donbosco, Upanga. Savio iliyowahi kuwa bingwa wa ligi hiyo ya BDL 2015, 2016, 2017, 2018 na 2021, ilishindwa kuonyesha makali yao kama ilivyozoeleka. Katika mchezo huo, ilionekana haijajianda vizuri…