Mida ya Simon Msuva kupiga mkwanja

MSHAMBULIAJI Simon Msuva anayekipiga Al Talaba ya Ligi Kuu ya Iraq, Iraq Stars League, anamaliza mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na inaelezwa anatakiwa na klabu za Misri na Saudi Arabia kutokana na kuvutiwa na kiwango chake. Nyota huyo wa zamani wa Wydad AC anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu baada…

Read More

Samatta Uefa ndo basi tena, arudi Europa League

KITENDO cha chama la nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, PAOK kushindwa kuingia nafasi mbili za juu kwenye michuano maalumu ya Super League ya Ligi Kuu ya Ugiriki, kimeikosesha tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa imeangukia Europa League. Samatta alikuwa anasaka nafasi nyingine ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada…

Read More

New King yavunja mwiko na kupanda ZPL 

Timu ya New King maarufu ‘Wachoma Mahindi’ imetegua kitendawili kilichokuwa kikiulizwa na wengi kwa miongoni mwa timu zilizopanda daraja na msimu ujao itacheza Ligi Kuu Zanzibar(ZPL). Timu nyingine zilivuka hatua hiyo kwa Kanda ya Pemba ni Wawi na Fufuni zitakazocheza ZPL kwa kwa mara ya kwanza pia.  Wachoma Mahindi wametinga hatua hiyo baada ya kuitandika mabao…

Read More

Dabi ya Kariakoo yapelekwa mkutano mkuu Yanga

BAADHI ya wanachama wa Klabu ya Yanga wamefikia hatua ya kuiandikia barua Kamati ya Utendaji kuomba kufanyika mkutano mkuu wa dharura kabla ya Juni 15, mwaka huu. Kwa mujibu wa Katiba ya Yanga, ili kuitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura inategemea idadi ya wajumbe waliopo na ridhaa ya kamati ya utendaji ya klabu au kwa…

Read More

Kisa Yanga, Simba yaweka mzigo mezani

VITA iliyopo hivi sasa kati ya Simba na Yanga katika Ligi Kuu Bara imemfanya kigogo mmoja wa Wekundu wa Msimbazi kuweka mzigo mezani kuhakikisha timu yao inafikia malengo. Simba ambayo leo, Jumapili inakabiliana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, tayari imeshuka dimbani mara 25, ikishinda 23, sare tatu na kupoteza mechi moja ikiachwa…

Read More

Tiketi ya CAF yampa presha kocha Azam FC

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema matokeo mabaya iliyopata timu hiyo katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Bara ni moja ya sababu za kuwarejesha haraka kambini wachezaji ili kujiandaa na mechi tatu za kufungia msimu zitakazoamua hatma yao ya CAF. Azam, iliyong’olewa mapema katika Ligi ya Mabingwa Afrika iliyoshiriki msimu huu…

Read More

JKT yachemsha Bara, ila kazi ipo huku

MAAFANDE wa JKT Tanzania kupitia kocha mkuu, Ahmad Ally wamekiri wamechemsha kwa kushindwa kufikia malengo ya Ligi Kuu ya kumaliza ndani ya 5-Bora, lakini kilichobaki kwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika Kombe la Shirikisho (FA) ili wakate tiketi ya Kombe la Shirikisho Afrika. JKT inayoshika nafasi ya saba kwa sasa imesaliwa na mechi tatu za…

Read More

Nyoni: Yanga ni bora, lakini inafungika

KIRAKA wa Namungo, Erasto Nyoni amefunguka kuwa hivi sasa wanaitazama zaidi Yanga ambayo ameitaja ni bora lakini inafungika. Namungo inatarajia kuwa ugenini dhidi ya Yanga, Mei 13 mwaka huu kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Katika maandalizi ya mchezo huo, Namungo imejichimbia Dodoma huku rekodi zikionesha…

Read More

Mechi tatu za heshima KenGold

LICHA ya KenGold kushuka daraja, lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Omary Kapilima amesema anataka kuacha maumivu ligi kuu kwa kuhakikisha anashinda michezo yote mitatu iliyosalia. KenGold inaburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi 16 ikiwa tayari imeshuka daraja baada ya kucheza mechi 27 ikishinda tatu, sare saba na vipigo 17, ndiyo…

Read More

Mtihani mgumu mrithi wa Ongala KMC

BAADA ya KMC kuachana na Kally Ongala, timu hiyo imemrejesha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Adam Mbwana Mubesh kukiongoza kikosi hicho hadi mwisho wa msimu, huku uongozi ukiweka wazi umempa uhuru wa kufanya kazi bila ya presha. Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula alisema wana imani kubwa na kocha huyo kwa…

Read More