Simba yaifuata Stade Malien na matumaini kibao

SIMBA inatarajiwa kuondoka alfajiri ya kesho Alhamisi Novemba 27, 2025 kwenda Bamako nchini Mali kuwahi pambano la pili la Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien, huku mastaa wa timu hiyo wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri baada ya awali kuanza na kichapo nyumbani mbele ya Petro Atletico. Simba inaondoka…

Read More

Simbu aifuata tuzo ya mwanariadha bora wa dunia Ufaransa

Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, kutoka timu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Staff Sajenti Alphonce Simbu, ameondoka nchini leo asubuhi Novemba 27, 2025 kuelekea Ufaransa kwa ajili ya kushiriki sherehe za tuzo za wanariadha bora wa mwaka 2025 zinazoandaliwa na Shirikisho la Riadha la Dunia. Hafla hiyo itafanyika Novemba 30, 2025 jijini Monaco nchini Ufaransa,…

Read More

Wasauzi waiokoa Yanga na figisu Algeria

UMESIKIA kilichoikuta Yanga huko Algeria? Basi kama hujui ni kwamba JS Kabylie watakaovaana nao Ijumaa Novemba 28, 2025 wameanza vitimbi mapema, lakini kama zali Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikawa mkombozi ikiwaokoa na figisu za kuzuiwa mabegi ya vifaa vya mazoezi. Yanga imeifuata JS Kabylie kwa ajili ya mechi ya Kundi B la Ligi ya…

Read More

Manula avunja ukimya Azam FC

BAADA ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu, kipa wa Azam FC, Aishi Manula amesema anapambana kwa nguvu kumshawishi kocha Florent Ibenge ampe nafasi kwani yupo tayari kuitumikia timu hiyo. Manula aliyerejea Azam msimu huu baada ya kumaliza mkataba akiwa na Simba, hajacheza mechi yoyote ya mashindano tangu atue hapo, huku kikosi hicho kikiwatumia makipa Zuberi…

Read More

Riadha Wanawake kurindima siku tatu Dar

MSIMU wa saba wa mashindano ya Riadha ya Wanawake utafanyika kuanzia Novemba 28, 2025 hadi 30, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yatakayofanyika kwa siku tatu, yatatanguliwa na semina kwa wanariadha na waamuzi itakayofanyika Novemba 28, 2025 uwanjani hapo. Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 26, 2025, Katibu Mtendaji…

Read More

Maabad aibuka shujaa Coastal ikitamba nyumbani

MSHAMBULIAJI wa Coastal Union, Maabad Maulid Maabad, ameibuka shujaa wa kikosi hicho kufuatia kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City. Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa leo Jumatano Novemba 26, 2025 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wenyeji Coastal Union iliingia ikiwa haijapata ushindi katika mechi nne zilizopita tangu mara ya…

Read More

Mkude anahesabu siku tu Singida BS

BAADA ya kukaa nje ya uwanja karibu nusu msimu, kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Jonas Mkude anahesabu siku tu kwa sasa kwani anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Singida Black Stars akiungana na Khalid Aucho waliyekipiga msimu uliopita wakiwa Jangwani. Ipo hivi. Mkude aliyependekezwa na kocha Miguel Gamond tangu mwanzoni  mwa msimu huu,…

Read More

Ratiba Ligi Bara yapanguliwa tena

IWAPO ulikuwa unadhani panga pangua ya ratiba ya Ligi Kuu Bara imemalizika baada ya wiki iliyopitwa kutangazwa mpya, basi pole yako, kwani Bodi ya Ligi (TPLB) imetangaza mabadiliko mengine kwa kuondoa mechi za Simba na Yanga. Simba na Yanga zinazotarajiwa kuendelea na mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika zikiwa ugenini, zilipangwa kurejea katika…

Read More