
Madagascar, Sudan mmetupa somo CHAN
KIJIWE kilipoa sana baada ya Taifa Stars kutolewa na Morocco katika robo fainali ya mashindano ya CHAN 2024 ambayo kesho Jumamosi yatafikia tamati. Hatuwezi kuchangamka na huku timu ambayo inasimama kama alama ya kutuunganisha Watanzania na mwenyeji, kuaga katika ardhi ya nyumbani. CHAN imetufunza mengi na miongoni mwa masomo tumeyapata kwa timu mbili za Madagascar…