Yanga kutesti  mitambo na Wakenya | Mwanaspoti

BAADA ya Rayon Sports, mastaa wa Yanga wanatarajia kushuka tena dimbani Septemba 12 wakiivaa Bandari ya Kenya kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi. Mara ya mwisho Yanga ilicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye tamasha hilo dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu Zambia msimu wa 2024/24 ikicheza na Red Arrow ikiibuka na ushindi wa mabao…

Read More

Straika la CHAN 2024 latajwa Uholanzi

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa la Algeria, Sofiane Bayazid ambaye amefunga mabao matatu kwenye mashindano ya CHAN 2024 ametajwa huko Uholanzi kwa kuhusishwa na Heracles inayoburuza mkia kwenye msimamo wa Eredivisie. Licha ya Algeria kuishia robo fainali kwenye michuano hiyo, Bayazid alionyesha kiwango kizuri kiasi cha kumezewa mate na Heracles ambayo imeanza msimu huu wa…

Read More

Oussama katika vita ya ufungaji CHAN 2024

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Morocco, Oussama Lamlioui, amekuwa silaha ya maangamizi kwa Morocco kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2024), huku akiwa katika nafasi nzuri ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora. Kabla ya mechi za nusu fainali ambazo zilipigwa leo Jumanne, Lamlioui alikuwa akiongoza orodha ya wafungaji akiwa…

Read More

Kiungo Sudan afichua siri za Appiah

KIUNGO wa timu ya taifa la Sudan, Abdel Raouf amefunguka kuhusu uhusiano wake na Kocha Kwesi Appiah, akiueleza kuwa ni zaidi ya kocha na mchezaji kwenye kikosi hicho ambacho jana, Jumanne kilicheza mechi ya nusu fainali ya CHAN dhidi ya Madagascar. Nyota huyo ambaye ni mchezaji wa Al-Hilal, alisema kocha huyo raia wa Ghana ni…

Read More

Penalti zaibeba Miembeni Yamle Yamle Cup

MIEMBENI imefuzu robo fainali ya michuano ya Yamle Yamle Cup inayoendelea kisiwani Unguja kufuatia ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Welezo City. Mchezo huo uliopigwa jana Jumatatu saa 12:30 jioni kwenye Uwanja wa Mao A, dakika tisini matokeo yalikuwa sare ya mabao 2-2. Wakasa Mbaraka aliitanguliza Miembeni kwa kufunga mabao mawili dakika ya 2 na…

Read More

SportPesa Tanzania yasaini upya udhamini wa Yanga: Mashabiki waupokea kwa shangwe ushirikiano huu mkubwa

Harakati kubwa kwenye anga la michezo nchini Tanzania ni huu si uvumi tu, bali ni uthibitisho wa dhamira ya kweli. Kupitia SportPesa Tanzania, kampuni inayoongoza michezo ya kubashiri kidijitali barani Afrika, imeimarisha nafasi yake si tu kwenye uwanja wa burudani, bali pia kwenye mustakabali wa soka la Tanzania. Hii ni zaidi ya mkataba; ni makubaliano…

Read More

Mrithi wa Kagere aahidi makubwa Namungo

MSHAMBULIAJI mpya wa Namungo, Herbert Lukindo amesema amejipanga vyema kuhakikisha anafanya vizuri na kikosi hicho na kuziba pengo la baadhi ya nyota walioondoka klabuni hapo akiwemo Meddie Kagere. Lukindo amejiunga na Namungo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KenGold ya Mbeya iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu msimu uliopita. Namungo imesafisha kikosi chake dirisha kubwa ikiachana…

Read More

Mgunda aongeza nguvu kambi ya Namungo

KOCHA wa Namungo, Juma Mgunda anajiandaa kutua kambini jijini Dodoma ikiwa ni siku chache tangu atoke katika majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili kuendelea na programu za kujiandaa na msimu mpya. Katibu wa timu hiyo, Ally Seleman alisema  Mgunda atajiunga na kambi iliyopigwa Dodoma na wachezaji walishaanza kufanya mazoezi chini ya…

Read More

Mbeya City yashusha mido Mnigeria

Mbeya City iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo raia wa Nigeria, Paschal Onyedika Okoli, ikiwa ni harakati za kukisuka kikosi hicho kwa msimu wa 2025-2026, kwa lengo la kuongeza na kuleta ushindani zaidi. Nyota huyo aliyezaliwa Oktoba 17, 1997, anakaribia kukamilisha dili hilo baada ya kuachana na Klabu ya NK Celik…

Read More