Watano Yanga wapewa siku saba

KAMBI ya Yanga imezidi kunoga kule Avic Town, Kigamboni Dar es Salaam, lakini jana ilikuwa katika mapumziko flani mafupi na kazi itaendelea leo Jumatatu, huku kocha wa timu hiyo, Romain Folz akitoa msimamo mzito ambao mabosi wa klabu wameafikiana nayo. Yanga iliamua kuahirisha…

Read More

Julitha Singano wa motoo Mexico

JANA beki wa Kitanzania, Julitha Singano alikiwasha kwenye mechi ya kirafiki kati ya Mexico All Stars na Barcelona Women, mechi iliyomalizika kwa sare ya 2-2. Singano anayekipiga FC Juárez, alikuwa mmoja wa wachezaji 20 wa Ligi ya Mexico waliochaguliwa kucheza mechi hiyo dhidi ya Barcelona, ambayo imekita kambi nchini humo kwa ajili ya maandalizi ya…

Read More

Ambundo ajiandaa kurejea Dodoma Jiji

ALIYEKUWA winga wa Fountain Gate, Dickson Ambundo anakaribia kurejea tena Dodoma Jiji, licha ya awali mabosi wa Mbeya City kufanya mazungumzo na nyota huyo na suala la masilahi binafsi ndilo lilifanya pande hizo kushindwana. Ambundo aliyemaliza mkataba wake na Fountain Gate huku kukiwa hakuna mazungumzo ya kuongeza mwingine, alikuwa akiongea na Mbeya City kwa ajili…

Read More

Kumekucha! Aucho aliamsha Singida Black Stars

AWALI ilielezwa kiungo raia wa Uganda, Khalid Aucho alikuwa mbioni kumfuata swahiba wake, Kennedy Musonda huko Israel alikoenda kucheza soka la kulipwa baada ya kumaliza mkataba na Yanga, lakini mwamba huyo alibadilisha gia angani. Aucho aliyeitumikia Yanga kwa misimu minne mfululizo, alimaliza mkataba…

Read More

CHAN 2024: Kocha Senegal afichua siri ya ushindi

KOCHA wa Senegal, Souleymane Diallo ameeleza maandalizi ya kisaikolojia kwa wachezaji wake na umakini katika utumiaji nafasi vilikuwa nguzo kuu ya ushindi wa timu yake dhidi ya Uganda katika mechi ya robo fainali ya mashindano ya CHAN 2024. Senegal ambao ni mabingwa watetezi wa mashindano hayo, walihitimisha safari ya timu ya mwisho ya ukanda wa…

Read More

Kriketi Tanzania yapania Kombe la Dunia T20

TIMU ya Taifa ya Kriketi ya Tanzania, imeanza mkakati wa kuitafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia ya mizunguko 20 (T20) inayoanza mwishoni wa juma, mjini Windhoek, Namibia. Tanzania iliibuka na ubingwa wa michuano ya kumbukumbu ya Kwibuka nchini Rwanda, baada ya kuifunga Zimbabwe katika fainali, huku Uganda ikishika nafasi ya tatu. Ikiwa na wachezaji…

Read More

FBSS, Lulanzi mabingwa Inter School Sports Bonanza

Timu ya mpira wa kikapu ya FBSS na ile ya soka ya Lulanzi zimetawazwa kuwa mabingwa katika mashindano ya 13 ya Inter School Sports Bonanza. Mashindano hayo yaliyofanyika Agosti 22, 2025 yalifanyika kwenye viwanja vya Filbert Bayi, mjini Kibaha yakishirikisha shule za Filbert Bayi (FBS) na shule jirani ikiwamo ya Lulanzi, Mkuza na Mwanalugali. Katika…

Read More

CHAN 2024: Staa Kenya ajifariji

NDOTO ya Kenya kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 imeishia hatua ya robo fainali, lakini kiungo Alpha Onyango ametoa matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo. Onyango alibeba tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya robo fainali dhidi ya Madagascar na kupoteza kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare…

Read More

Taji la 2025 ni mbio za farasi wawili

MBIO za kusaka taji la ubingwa wa Taifa wa mbio za magari zimezidi kupata sura mpya baada ya bingwa mtetezi, Manveer Birdi kurudi upya na kutishia uongozi wa dereva kutoka Arusha, Gurpal Sandhu. Sandhu ambaye alikuwa mbele ya Manveer Birdi kwa pointi 21 kabla ya kwenda Morogoro alikuwa akiongoza kwa pointi 56, huku Birdi na…

Read More

Konde Boy kucheza Ligi Kuu Misri

KINDA wa Azam FC, Arafat Masoud ‘Konde Boy’ (18), amejiunga na ENNPI ya Ligi Kuu Misri kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kudumu kwa miaka minane Chamazi. Kinda huyo alijiunga na Azam mwaka 2017 akicheza timu za vijana za U-17 na U-20 kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa na msimu uliopita aliichezea Fountain Gate…

Read More