
Konde Boy kucheza Ligi Kuu Misri
KINDA wa Azam FC, Arafat Masoud ‘Konde Boy’ (18), amejiunga na ENNPI ya Ligi Kuu Misri kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kudumu kwa miaka minane Chamazi. Kinda huyo alijiunga na Azam mwaka 2017 akicheza timu za vijana za U-17 na U-20 kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa na msimu uliopita aliichezea Fountain Gate…