Taji la Kagame lampa mzuka Gamondi

KOCHA Mkuu wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi amesema taji la Kagame walilolitwaa litakuwa chachu ya kuiweka timu kwenye morali nzuri kuikabili Rayon Sports Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu. Gamondi alifunguka hayo saa chache baada ya timu yake ikiwa na nyota 26 kuanza safari ya kwenda Rwanda kuwafuata wapinzani wao kwenye michuano ya Kombe la…

Read More

Nyota Twiga Stars apata dili Uturuki

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, Noela Luhala amejiunga naAntalyaSpor 1207 inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki. Noela ambaye msimu uliopita alikuwa akicheza Asa Tel Aviv ya Israel, alisafiri kwenda Uturuki jana tayari kuanza kuitumikia timu hiyo aliyosaini nayo mkataba wa mwaka mmoja ambao una kipengele cha kumruhusu kuondoka ifikapo Januari…

Read More

Kaizer Chiefs, Nabi shughuli imeisha

Taarifa kutoka Afrika Kusini zinabainisha kuwa, Kaizer Chiefs imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha wake, Nasreddine Nabi. Ripoti mbalimbali zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini humo zinabainisha sababu ya Kaizer Chiefs kufikia uamuzi huo ni baada ya kubainika Nabi leseni yake ya ukocha ya CAF imekwisha muda wa matumizi, hivyo kumfanya asikubalike kuongoza timu…

Read More

Hongera JKT Queens, Kenya wakubali tu

KIJIWE kinawapongeza Maafande wetu wa kike JKT Queens kwa kuibuka mabingwa wa mashindano ya kuwania kufuzu Klabu Bingwa Afrika 2025 yaliyofikia tamati Jumanne wiki hii huko Kenya. Kwa kutwaa huko ubingwa, JKT Queens imejihakikishia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake, shindano ambalo wiki kama mbili au tatu zijazo litafanyika Algeria likishirikisha klabu…

Read More

Taifa Stars yaanguka nafasi nne viwango FIFA

Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanguka kwa nafasi nne katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) vilivyotangazwa leo, Septemba 18, 2025. Tanzania imedondoka kwa nafasi kutoka ya 103 ambayo ilikuwepo awali hadi nafasi ya 107 kwa viwango vilivyotolewa leo na FIFA. Kufanya vibaya…

Read More

Bado Watatu – 32 | Mwanaspoti

NIKAMJIBU: “Sikutaka nikupe mshituko. Nilikuwa nakungoja urudi.”“Mimi nimepata habari hii leo wakati narudi.”“Ni nani aliyekupa habari hiyo?”“Ni mke wake. Alinipigia simu akanijulisha hivyo. Nikashituka sana kwa sababu juzi juzi tu nilikuwa naye. Kwa hiyo nilipofika stendi nikaona niende huko kwanza nikampe pole.”“Hata mimi nilishituka, yaani mpaka hivi sasa picha yake inanijia akilini mwangu!”“Kushituka ni lazima….

Read More

Ibenge kuifikisha Azam nchi ya ahadi?

TANGU msimu wa 2013-14 ambao Azam FC ilibeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mara ya kwanza kwao, wamepita makocha mbalimbali kuifukuzia rekodi hiyo, wameshindwa. Mzigo huo sasa umeangukia kwa Florent Ibenge, kocha mwenye rekodi kubwa katika soka la Afrika kutokana na kushinda mataji yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Ibenge…

Read More

Kinapigwa leo Dabi ya Wanajeshi Lgi Kuu Bara

LIGI Kuu Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa, huku mechi ya mapema ikiwa ni saa 8:00 mchana kati ya Fountain Gate itakayoikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara, lakini pia kuna Dabi ya Wanajeshi, Mashujaa dhidi ya JKT Tanzania. Fountain Gate inaingia katika mchezo huo ikiwa ni timu ambayo…

Read More

Mambo 10 Dabi ya Kariakoo, tatizo ni Diara!

DABI ya kwanza ya Kariakoo msimu huu imemalizika kibabe baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, juzi Jumanne. Ushindi huo umeifanya Yanga, kuendeleza ubabe mbele ya Simba, ikishinda mchezo wa sita mfululizo dhidi ya watani wao hao, rekodi ambayo itaendelea kuwafanya Wekundu kuumizwa na maumivu mithili ya kidonda kisichopona. Hata…

Read More