Folz afanya maamuzi mazito Dar

KAMA ulikuwa hufahamu kuna miezi kadhaa Yanga ilikuwa inajifua ikitumia viwanja vya kukodi, lakini juzi kikosi hicho kilirudi rasmi kambi yao iliyozoelekea lakini iliyokarabatiwa upya pale Avic Town, Kigamboni, jijini Dar es Salaam baada ya kocha wa timu hiyo, Romain Folz kufanya maamuzi. …

Read More

Abdi Banda asaini Dodoma Jiji

BEKI wa zamani wa Simba na Coastal Union, Abdi Banda, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia Dodoma Jiji baada ya ule wa miezi sita kumalizika msimu huu. Nyota huyo alijiunga na kikosi hicho Januari 15, 2025 akitokea Baroka FC ya Afrika Kusini, ambako alivunja mkataba miezi mitatu baada ya kuipeleka FIFA timu ya Richards…

Read More

Hongera Simba Queens kwa kujivua gamba usajili

KATIKA dirisha linaloendelea la usajili, Simba Queens imejilipua hasa kwa kuacha majina mengi makubwa ambayo mengine hayakutegemewa kama yangeweza kupigwa chini. Mfungaji Bora wa kikosi hicho kwa msimu uliopita, Jentrix Shikangwa ni miongoni mwa mastaa ambao wamepewa mkono wa kwaheri na Simba Queens ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya…

Read More

Malijendi wakoshwa na kiwango CHAN

MASHINDANO ya msimu huu ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2024) yametajwa kuwa bora zaidi kiushindani na wajumbe wa masuala ya kiufundi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF TSG) na yameonyesha maendeleo makubwa kuliko yaliyopita. Wajumbe hao, akiwemo Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ethiopia, Abraham Mebratu na mchezaji wa…

Read More

CHAN 2024: CAF yazuia wapigaji Uganda

WAKATI timu ya taifa ya Uganda Cranes ikijiandaa kwa mechi ya nusu fainali ya CHAN 2024 dhidi ya Senegal, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechukua hatua ya kupunguza idadi ya tiketi ambazo shabiki anaweza kununua mtandaoni. Hadi sasa, kila shabiki ataruhusiwa kununua tiketi tatu tu, kutoka tano zilizokuwa zikiruhusiwa awali. Taarifa hiyo imetolewa na Dennis…

Read More

Namba zaibeba Stars, hesabu za robo zikianza

KATIKA msimu huu wa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2024), takwimu zimeonyesha kuwa timu ya taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ ndio timu iliyofanya vizuri zaidi katika hatua ya makundi ambayo ilitamatika juzi, Jumanne kwa mechi mbili za kundi D. Katika mechi hizo, zilishuhudiwa Sudan na Senegal zikiungana na wenyeji, Tanzania,…

Read More

Dante mbioni kutua Kagera Sugar

BAADA ya aliyekuwa beki wa kati Andrew Vincent ‘Dante’ kuachana na KMC kutokana na mkataba kumalizika, kwa sasa yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Kagera Sugar. Dante aliyeitumikia KMC kwa miaka mitano, huku akizichezea pia Yanga na Mtibwa Sugar kwa nyakati mbalimbali, anafanya mazungumzo hayo ya kujiunga na Kagera Sugar ambayo kwa msimu…

Read More

Mkandala awindwa Coastal Union | Mwanaspoti

UONGOZI wa Coastal Union uko katika mazungumzo ya kumsajili aliyekuwa nyota wa Kagera Sugar FC, Cleophace Mkandala baada ya kiungo huyo kumaliza mkataba, huku kukiwa hakuna mazungumzo ya kuongeza mwingine mpya wa kukichezea pia kikosi hicho. Nyota huyo wa zamani wa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, ameamua kutafuta changamoto sehemu nyingine…

Read More