
Waandishi, wadau wa habari wamlilia Sharon, wamtaja mwalimu aliyeondoka
Dodoma. Mwandishi mwandamizi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Sharon Sauwa amefariki dunia. Sharon amekutwa na umauti alfajiri leo Agosti 19, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Kifo chake kimepokewa kwa mshtuko na wanahabari wenzake na wadau wa habari, ambao wamemweleza kama mtu aliyekuwa mwalimu na kiongozi wa kipekee katika…