Simba yajivunia jezi mpya, Mangungu akiweka angalizo

WAKATI Simba ikitamba kuwa jezi zao mpya zinazozinduliwa leo Agosti 31, 2025 zitakuwa za ubora wa hali ya juu, mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amewataka mashabiki na wanachama kuilinda chapa yao. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo unaofanyika leo katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar, Mangungu amesema kuwa jezi zao ni…

Read More

Mbwana Samatta mdogo mdogo Ligue 1

NAHODHA wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ameendelea kuizoea Ligi Kuu ya Ufaransa, baada ya usiku timu anayoichezea ya Le Havre kupata ushindi wa kwanza wa mabao 3-1 dhidi ya Nice. Katika mechi hiyo ya Ligue 1, nyota huyo wa kimataifa wa Tanzania alitumika kwa dakika 85, wakati timu ikiwa tayari inaongoza kwa…

Read More

Akandwanaho, Chobwedo wailiza Fountain Gate

MABAO mawili yaliyofungwa na Joseph Akadwanaho na Ramadhan Chobwedo, yametosha kuipa furaha Tabora United na kupeleka kilio Fountain Gate. Hiyo ilikuwa katika mchezo wa kwanza wa Kundi A kwenye michuano ya Tanzanite Pre-Season International iliyoanza leo Agosti 31, 2025. Michuano hiyo inayofanyika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manywara, Akandwanaho alianza kuifungia Tabora United…

Read More

Tanzania ya pili Kombe la Dunia la vijana wa mazingira magumu

Timu ya Tanzania ya Wanawake kutoka kituo cha Future Stars Academy cha jijini Arusha, imeshika nafasi ya pili katika michuano ya vijana wanaotoka kwenye mazingira magumu (Homeless World Cup) yaliyofanyika kati ya Agosti 22-30 jijini Oslo, Norway, yakishirikisha timu 60 kutoka mataifa 48. Future Stars Academy imetwaa nafasi hiyo baada ya kushinda mchezo wa fainali…

Read More

Simba, Yanga zabanwa, kisha zalainishiwa Bara

VIGOGO vya soka nchini, Simba, Yanga na Azam FC wamelainishwa mambo katika ishu za usajili, lakini wakabanwa kwa upande mwingine katika Ligi Kuu Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) kwa msimu mpya wa 2025-26. Msimu huo unatarajiwa kuzinduliwa na mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Septemba 16 Kwa Mkapa ikizikutanisha Simba na Yanga…

Read More

Haroun Mandanda kutua Polisi Tanzania

TIMU ya maafande wa Polisi Tanzania iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa aliyekuwa kipa wa kikosi cha Tabora United, Haroun Mandanda baada ya kumaliza mkataba, huku kukiwa hakuna mazungumzo ya kuongeza mwingine. Nyota huyo aliyetamba na timu mbalimbali za Mbeya City, Ihefu (Singida Black Stars) kisha baadaye pia kujiunga na Tabora United,…

Read More

Mgaza aiokoa Dodoma Jiji dakika za jioni

WAKATI Tanzania Prisons ikiwa na matumaini ya kuondoka na pointi tatu, mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Yassin Mgaza dakika ya mwisho akaiokoa timu hiyo na kichapo katika mechi ya kwanza wa mashindano ya Tanzanite Pre-Season International. Mchezo huo ulioanza kupigwa  saa 7:00 mchana leo Agosti 31, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, kipindi cha kwanza kilimalizika…

Read More

Samatta, Gomes waitwa Taifa Stars

NAHODHA na nyota wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga, Le Havre ya Ufaransa, Mbwana Samatta na mshambuliaji mpya wa Simba, Seleman Mwalimu ‘Gomes’ ni miongoni mwa wachezaji waliotwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kilichotangazwa rasmi leo Jumapili. Kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amekitaja kikosi hicho kwa ajili ya kambi ya…

Read More