Tuzo yampa nguvu staa Mashujaa

ABDULRAHMAN Mussa ambaye anatumika kama beki wa kulia ndani ya kikosi cha Mashujaa, amesema tuzo aliyoipata katika mchezo dhidi ya Coastal Union imempa nguvu mpya ya kuendelea kupambana. Mussa ambaye pia ana uwezo wa kucheza kiungo mshambuliaji, juzi Ijumaa alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union iliyochezwa kwenye…

Read More

Uhamiaji, Kipanga zaangukia pua ZPL

WAKATI maafande wa Zimamoto na JKU wakishuka uwanjani jioni ya leo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Zanzibar, juzi Kipanga na Uhamiaji zilipata aibu baada ya kufungwa, huku Mlandege ikibanwa na wageni Junguni nyumbani, kwenye Uwanja wa Amaan B, mjini Unguja. Kipanga ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Gombani, ilifumuliwa na Mwenge mabao 2-1,…

Read More

Patrick Aussems aanza kunogewa Bara

LICHA ya kuwa na mwanzo mzuri katika Ligi Kuu Bara, Singida Black Stars wanajua bado wana kazi kubwa mbele yao. Kocha wa timu hiyo, Patrick Aussems amesema licha ya kupata pointi tisa katika michezo mitatu iliyopita, anahitaji kuhakikisha kikosi chake kinakuwa bora zaidi. Katika michezo mitatu iliyopita, Singida Black Stars ilivuna pointi sita ugenini baada…

Read More

TFF, waamuzi wamlilia Abdulkadir | Mwanaspoti

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Waamuzi wa Soka Tanzania (FRAT) wameonyesha masikitiko yao kutokana na kifo cha aliyekuwa mwamuzi mstaafu na mwenyekiti wa Frat, Omary Abdulkadir. Abdulkadir aliyezikwa leo mchana katika makaburi ya Kisutu, alifariki dunia jana usiku kutokana na maradhi ya figo. TFF imemwelezea Abdulkadir kama miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa…

Read More

Namungo, Mgunda suala la muda

KOCHA msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda huenda kuna kitu kikatokea baina yake na Namungo, baada ya timu hiyo kurudi tena kuzungumza naye, ili kukinoa kikosi chao, tetesi zikisema ni suala la muda kumfuta kazi, Mwinyi Zahera. Msimu uliopita, Zahera aliisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya sita, ikivuna pointi 36, ingawa alijiunga nayo katikati ya…

Read More

Ngushi aibeba Mashujaa, Coastal Union hoi

Bao la mshambuliaji Crispin Ngushi, limetosha kuipa ushindi wa pili Mashujaa, ikiendeleza makali yake kwenye Ligi Kuu Bara ikiwalaza Coastal Union ya Tanga. Ngushi amefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akipokea pasi ya beki Abderhman Mussa, kisha mfungaji kuwatoka kiakili mabeki na kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Ley Matampi wa Coastal Union….

Read More

Mdamu afanyiwa upasuaji | Mwanaspoti

HATIMAYE aliyekuwa mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Gerald Mathias Mdamu, amefanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia ambao ulikumbwa na changamoto ya jipu la kwenye mfupa. Mdamu alipata ajali ya kuvunjika miguu Julai 9, mwaka 2021, akiwa na wenzake katika basi la timu ya Polisi Tanzania likitokea mazoezini katika Uwanja wa TPC wakienda kambini, ambapo alifanyiwa upasuaji…

Read More

Jeuri ya Simba CAFCC ipo hapa

WACHEZAJI wa Simba wanafahamu hesabu zilizopo kwao hivi sasa ni kuanza vizuri ugenini dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya kisha kumaliza kazi nyumbani na kutinga makundi. Jeuri kubwa waliyonayo Simba ni maboresho ya kikosi chao ambacho msimu huu kimeanza ligi kwa ushindi wa asilimia 100 kutokana na kukusanya pointi sita katika mechi mbili walizocheza…

Read More

Dube, Pacome wamtisha kocha CBE

WAKATI Yanga ipo tayari katika ardhi ya Ethiopia kwa mechi ya mkondo wa kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha wa wenyeji ameibuka na mambo matatu mazito aliyoyasoma kwa kikosi hicho cha Jangwani. Kocha Sisay Kebede Kumbe wa CBE SA ya Ethiopia itakayokutana na Yanga kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Abebe…

Read More

Shuti la Fei Toto Lamtingisha kipa Simba

KIPA wa Simba, Moussa Camara ‘Spider’ alikuwa katika benchi wakati taifa lake la Guinea likiachia pointi tatu mbele ya Taifa Stars, lakini akaondoka na lile shuti la kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambalo lilizaa bao la kusawazishia kabla ya Mudathir Yahya kufunga la ushindi kwa Tanzania. Fei Toto alifunga bao hilo kwa…

Read More