Job asimulia mazito Ivory Coast

BEKI wa Taifa Stars, Dickson Job amesimulia mazito juu ya majeraha yake wakati alipotolewa kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Guinea, huku akiwatoa hofu mashabiki wa Yanga anayoitumikia. Job aliumia dakika ya tisa ya mchezo huo baada ya kugongana na kiungo wa Guinea na kulazimika kutolewa dakika ya 11 nafasi yake ikichukuliwa na Bakari…

Read More

Simba yafukua faili la Mpanzu

KAMA uliona bado mapema kwa Simba kutafuta mchezaji wa kumsajili dirisha dogo msimu huu, basi umekosea, kwani Wekundu hao wamegonga hodi tena kwa Winga Mkongoman Elie Mpanzu, huku mwenyewe akifunguka na kuwataja mabosi wa Msimbazi. Winga huyo aliyekuwa akiichezea AS Vita kabla ya kutimkia Ubelgiji, aliwahi kuhitajika na Simba lakini aliamua kuwakacha kweupe akitoa sababu…

Read More

Arusha yafungua fursa ya michezo kwa wadau

Halmashauri ya Jiji la Arusha imeonyesha nia ya kushirikiana na wadau pamoja na vituo vya kuibua na kulea vipaji vya michezo ili kutoa nafasi kwa vijana kutimiza ndoto na malengo yao. Hayo yamesemwa na Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Abraham Mollel wakati akifungia tamasha la michezo kwa vijana walio chini ya umri wa miaka…

Read More

Morocco na tumaini la Stars Afcon 2025

KAIMU kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco, ameleta matumaini mapya kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania. Tangu achukue mikoba ya kuinoa Taifa Stars baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Adel Amrouche wa Algeria kufungiwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Morocco ameonyesha uwezo mkubwa wa kuiongoza timu…

Read More

Tabora Utd yalizamisha jahazi la Kagera mchana

JAHAZI la Kagera Sugar linazidi kuwenda mrama baada ya mchana wa leo kufumuliwa bao 1-0 na Tabora United, ikiwa ni kipigo cha tatu mfululizo kwa timu hiyo inayonolewa na kocha kutoka Uganda, Paul Nkata. Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa Nyuki wa Tabora, baada ya awali kuitungua Namungo ikiwa ugenini mjini Lindi kwa mabao…

Read More

Mdamu aanza matibabu Moi | Mwanaspoti

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Wallace Karia, limetekeleza ahadi liliyoitoa wikiendi iliyopita kwa mshambuliaji wa zamani wa Polisi Tanzania, Gerald Mdamu kumlipia gharama za matibabu, ambapo nyota huyo ni kama ameanza maisha mapya baada ya mateso ya zaidi ya miaka miwili. Julai 9, mwaka 2021, basi la Polisi Tanzania lilipata ajali likitoka…

Read More

Mziki wa Hamza Simba washtua mastaa

KIWANGO alichokionyesha beki wa Simba, Abdulrazack Hamza katika mechi tatu dhidi ya Coastal Union (Ngao ya Jamii), Tabora United na Fountain Geti za Ligi Kuu, kimewaibua baadhi ya mastaa wa timu za Ligi Kuu kumzungumzia wakisema akiendelea kukomaa atamnyang’anya mtu namba kikosini. Beki huyo aliyesajiliwa na Simba msimu huu kutoka Cape Town United ya Afrika…

Read More

Makambo aja na jipya Ligi Kuu Bara

MSHAMBULIAJI wa Tabora United, Heritier Makambo ‘Mzee wa Kuwajaza’ amesema kuna mabadiliko makubwa ya ubora katika Ligi Kuu Bara kulinganisha na misimu kadhaa nyuma alipokuwa na kikosi cha Yanga. Makambo ameitumikia Yanga kwa misimu miwili tofauti baada ya kuuzwa Horoya ya Guinea na baadaye akarejea tena nchini na kuondoka kwenda Uarabuni kabla ya hivi karaibuni…

Read More