Mkenya awatoa hofu Pamba, aahidi pointi 3 Azam

LICHA ya kutopata ushindi kwenye mechi tano na kufunga mabao mawili pekee, Nahodha wa Pamba Jiji, Christopher Oruchumu amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akisisitiza ni kipindi cha mpito na kwamba itaanza kufanya vizuri kuanzia mchezo ujao dhidi ya Azam FC. Mechi tano za Pamba Jiji tangu Agosti, mwaka huu, chini ya Kocha Goran Kopunovic…

Read More

Ngoma, Fadlu kumekucha | Mwanaspoti

MAISHA ndani ya Simba yanakwenda kasi na siku zinasonga, kwani misimu minne iliyopita walikuwa wakitamba nchini wakiwa ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam (FA) na pia Ngao ya Jamii, na mambo Msimbazi yalikuwa byee! Lakini, baada ya watani zao, Yanga kujipanga na kuja na mziki mpya mambo yalianza kubadilika Msimbazi,…

Read More

Hesabu mpya za Yanga kwa Wahabeshi

WAKATI kesho Alhamisi kikosi cha Yanga kikitarajia kusafiri kuelekea Ethiopia, kuna matumaini yapo kwao ya kufanya vizuri ugenini kabla ya kurudi nyumbani kumalizia kazi. Kikosi hicho kinakwenda kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza dhidi ya CBE SA ambao utachezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Abebe Bikila uliopo Addis Ababa…

Read More

Taifa Stars yatamba ugenini ikiichapa Guinea

Taifa Stars imeitoa kimasomaso Tanzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Guinea katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 iliyochezwa katika Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro, Ivory Coast. Guinea walikuwa wa kwanza kupata bao katika 57 kupitia kwa Mohamed Bayo. Bayo alifunga bao hilo…

Read More

Mambo matatu yanayoibeba Simba kwa Al Ahli Tripoli

Dar es Salaam. Timu ya Simba inatarajiwa kushuka uwanjani Jumapili ijayo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaopigwa nchini Libya dhidi ya Al Ahli Tripoli. Al Ahli inakutana na Simba baada ya kuiondosha Uhamiaji ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 5-1, ambapo mchezo wa kwanza ilishinda mabao 2-0 kabla…

Read More

Kagera Sugar yatambia rekodi kwa Tabora United

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Paul Nkata, raia wa Uganda amesema baada ya kucheza michezo miwili ya ligi na kupoteza yote, sasa wamejipanga kupambana kufa au kupona ili kuanza kukusanya pointi huku akiamini kwamba rekodi ya msimu uliopita itawabeba dhidi ya Tabora United. Kauli ya kocha huyo imekuja ikiwa kesho Jumatano anatarajia kukiongoza kikosi chake…

Read More

Geay ageukia New York Marathon

BAADA ya kushindwa kutamba katika marathoni za Olimpiki zilizofanyika Paris, Ufaransa mwaka huu, mwanariadha Gabriel Geay amesema kuwa nguvu zote kwa sasa amezielekeza kwenye mbio za New York City Marathon. Akizungumza na Mwanaspoti, Geay alisema japokuwa ni mara ya kwanza kushiriki mbio hizo, lakini anaamini atakwenda kufanya vizuri kulingana na namna ambavyo anaendelea kufanya mazoezi….

Read More

Young Profile yaipoteza Crossover | Mwanaspoti

TIMU ya Young Profile imeifunga Crossover kwa pointi 52-49 katika Ligi ya Kikapu Mwanza kwenye mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mirongo mjini humo. Ushindi wa Young Profile ulitokana na muda wa nyongeza ulioongezwa baada ya timu hizo kufungana pointi 43-43 katika robo zote nne. Baada ya dakika tano kuongezwa, Young Profile ilianza mchezo kwa kasi…

Read More

Gidabuday kuzikwa Jumamosi Katesh | Mwanaspoti

MWILI wa Wilhelim Gidabuday utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Jumamosi kijijini kwao Nangwa, Katesh. Gidabuday aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), amefariki alfajiri ya kuamkia jana Septemba 10, 2024 baada ya kugongwa na gari jijini Arusha. Mdogo wa marehemu, Julius Gidabuday alisema safari ya kwenda Katesh mkoani Manyara itaanza Ijumaa…

Read More

Risasi, Kahama Sixers freshi | Mwanaspoti

RISASI na Kahama Sixers zimeianza vizuri kampeni ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Shinyanga baada ya kushinda katika hatua ya kwanza ya nusu fainali. Katika mchezo wa kwanza Risasi iliishinda Veta kwa pointi 12-80, huku Kahama Sixers ikifunga B4 Mwadui kwa pointi 80-75. Akizungumza na Mwanaspoti, Kamishina wa Ufundi na Mashindano wa…

Read More