
Madagascar yaifumua Burkina Faso ikiifuata Stars robo fainali
TIMU ya taifa ya Madagascar imeungana na Taifa Stars kutinga robo fainali ya mashindano ya CHAN, baada ya kuifunga Burkina Faso mabao 2-1, kwenye Uwanja wa New Amaan Stadium, Zanzibar. Matokeo hayo yameifanya Madagascar kuizidi kete Mauritania iliyokuwa ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi B, kabla ya Madagascar kuibuka na ushindi huo muhimu…