MCC yaanza kibabe kriketi TCA

SEPTEMBA imeanza vyema kwa timu ya MCC ya kriketi iliyoshinda kwa mikimbio 83 dhidi ya Caravans D katika mchezo wa Ligi ya TCA ya mizunguko 20 iliyopigwa jijini Dar es Salaam. Kumzidi mpinzani kwa mikimbio 83 ni ushindi mkubwa na mashujaa walikuwa Gokul Nair aliyekuwa na mikimbio 64 na Roshan Gaussian 59 kwa washindi. “Ni…

Read More

Taifa Stars ilijikaba yenyewe kwa Wahabeshi

TAIFA Stars imeanza mbio za kusaka tiketi ya kwenda katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwakani huko Morocco, kwa kudondosha pointi mbili nyumbani mbele ya timu ya Ethiopia kwa kulazimishwa suluhu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Katika mechi hiyo ya Kundi H iliyopigwa janai usiku, Stars ilishindwa…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Usia wangu kwa Kocha Liogope

RAFIKI yangu Kassim Liogope amepewa jukumu zito la kukaimu nafasi ya ukocha mkuu wa Azam FC muda mfupi baada ya timu hiyo kumtimua kocha Youssouph Dabo. Kabla ya kubebeshwa mzigo huo, Liogope alikuwa akifundisha kikosi cha vijana cha Azam na alinasa kibarua hicho baada ya Dodoma Jiji aliyoitumikia msimu uliopita akiwa kocha msaidizi kuamua kutompa…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Tusiikatie tamaa Taifa Stars Afcon

MWANZO haujawa mzuri kwa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars katika mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 ambazo zitafanyika huko Morocco, mwakani. Mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali hizo katika kundi H dhidi ya Ethiopia ambao tulikuwa nyumbani, Jumatano iliyopita ulimalizika kwa sare tasa kwenye…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Zahera bado hayupo salama Namungo

MWINYI Zahera mwanzoni mwa wiki hii alipitia katika kikaango baada ya kuponea chupuchupu kutimuliwa na Namungo kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo, Baada ya Namungo kupoteza mchezo dhidi ya Fountain Gate kwa mabao 2-0 nyumbani, kocha huyo alikutana na kadhia ya mashabiki wa timu hiyo ambapo alirushiwa makopo kwenye Uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa,…

Read More

Dili la Badru lakwama Songea United

ALIYEKUWA kocha wa timu za vijana za Azam FC, Mohammed Badru amesema dili lake kutua Songea United limeota mbawa na badala yake imembidi kutoa sapoti kwa viongozi wa chama hilo kutokana na heshima yao kwake, hivyo ilimbidi kuandaa programu mbalimbali za mazoezi kama sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya msimu ujao wa Championship. Badru…

Read More

Ilanfya majanga, nje wiki mbili

MSHAMBULIAJI wa JKT Tanzania, Charles Ilanfya yamemkuta baada ya kuelezwa atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili hadi uvimbe wa goti alionao upungue ndipo aanze vipimo ili kugundua tatizo linalomsumbua baada ya kuumia walipocheza dhidi ya Azam, Agosti 28, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Ilanfya alisema baada ya kupata maumivu goti…

Read More

Aucho afichua kinachoibeba Ligi Kuu Bara CECAFA

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Khalid Aucho kwa sasa yupo katika kambi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes, huku akifichua kinachoibeba Ligi Kuu Bara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Aucho maarufu kama Dokta, amesema uwekezaji ndiyo sababu kubwa ya Ligi Kuu Bara kuwa na ushawishi kwa nchi nyingine kuifuatilia na kushabikia baadhi…

Read More

Sanawe: Sasa ni ubaya ubwela tu

WAKATI timu tano zikipambana kujinasua zisishuke daraja katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD), baadhi ya makocha wa timu hizo wamesema kwa sasa walipofikia ni kuombeana mabaya. Timu hizo ni KIUT, Jogoo, Ukonga Kings, Mgulani JKT, huku timu tatu ndizo zinatakiwa kushuka daraja. Wakiongea kwa nyakati tofauti na Mwanaspoti makocha hao walisema…

Read More

Dar City yachemsha kwa maafande BD

TIMU ya JKT iliwashangaza wengi pale ilipoifunga timu ngumu ya Dar City kwa pointi 83-66 katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD) iliyofanyika kwenye Uwanja wa Donbosco Oysterbay. Dar City itabidi ijilaumu yenyewe kupoteza mchezo huo kutokana na kushindwa kutegua mfumo wa uchezaji uliotumiwa na timu ya JKT. Mfumo uliotumiwa na JKT…

Read More