
Freddy arudi ghafla, ajifua na mastaa wa Yanga
BAADA ya kusepa Simba, mshambuliaji Freddy Kouablan amerejea nchini kimya kimya, lakini akashtua kujifua na mastaa wa Yanga. Freddy ambaye alitua Simba dirisha dogo msimu uliopita akitokea Green Eagles ya Zambia akiwa amefunga mabao 11 yaliyomfanya awe Mfungaji Bora mwishoni mwa msimu wakati akiwa Msimbazi, aliondoka Simba hivi karibuni kumpisha Leonel Ateba kutoka USM Alger…