
Mavambo aipa jeuri Simba SC
MSIMU uliopita, ungemwambia shabiki wa Simba kwamba mabosi wa klabu yake watamuacha kiungo wao Fabrice Ngoma wangeweza kukutia ngumi achilia mbali kung’aka kwa mshtuko. Lakini mechi mbili tu ndani ya msimu mpya ukiongeza na zile dakika 45 alizocheza katika Simba Day, zimetosha kumuibua mfalme mpya wa eneo la kiungo cha ulinzi, Debora Fernandes Mavambo. Huwaambii…