Aliyezuia usajili Fountain Gate huyu hapa

Mabosi wa Fountain Gate, bado wanahaha kunusuru usajili ili kuanza msimu mpya, lakini kama unataka kumjua staa aliyezuia usajili ni Rodrigo Figueiredo Calvalho. Fountain Gate imeshindwa kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, kutokana na madai ya kusitishiwa mkataba kwa Rodrigo, raia wa Brazil. Mshambuliaji huyo ambaye aliitumikia timu hiyo kwa…

Read More

MVP Simba awatoa hofu mashabiki

BAADA ya Simba kuanza Ligi Kuu Bara kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United, kiungo wa mpya wa kikosi hicho, Ahoua Charles amewatoa hofu mashabiki wao akisema hana presha na kiwango chake wala kikosi na ni suala la muda tu mambo yatakuwa matamu zaidi. Katika msimu wa 2023/24 Ahoua aliibuka mchezaji bora…

Read More

Chama aandika rekodi tatu CAF, amfukuzia Tresor Mputu

BAO moja la Clatous Chama katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga iliupata dhidi ya Vital’O ya Burundi, Jumamosi iliyopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika, limemfanya kuandika rekodi mbili huku akiboresha nyingine ya tatu. Chama alifunga bao dakika ya 68 akiunganisha mpira uliogonga mwamba na kurudi uwanjani ambao ulitokana na shuti lililoupigwa na Stephane Aziz…

Read More

Enekia aanza kutupia Mexico | Mwanaspoti

SIKU chache tu tangu atambulishwe Mazaltan FC ya Mexico, nyota wa kimataifa wa Tanzania, Enekia Lunyamila amefunga bao kwenye mchezo wa ligi ya Sweden na kuipatia ushindi timu hiyo. Lunyamila alitambulishwa Mazaltan akitokea Eastern Flames ya Saudia ambayo ilimaliza nafasi ya saba kati ya timu nane zinazoshiriki Ligi ya Wanawake nchini humo. Msimu uliopita Mazaltan…

Read More

Sababu ya Warriors Queens kujiondoa Cecafa

KATIBU Mkuu wa Warriors Queens ya Zanzibar, Neema Othman Machano amesema sababu ya kujiondoa kwenye mashindano ya Cecafa kwa wanawake ngazi ya klabu ni changamoto ya kifedha ikiwemo usafiri. Michuano hiyo ya kuwania nafasi ya kuuwakilisha Ukanda wa Cecafa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake ilianza juzi ambapo Tanzania ilitarajiwa kuwakilishwa na timu…

Read More

Dabo asaka dawa ya APR

KAULI ya Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo kuhusu wapinzani wake APR imeonekana kuwa na maswali mengi juu ya kitakachoenda kutokea katika mchezo wa marudiano jijini Kigali nchini Rwanda. Juzi Jumapili Azam iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kwanza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa…

Read More

Tabora United na rekodi mbovu mechi 16 ugenini

KICHAPO cha mabao 3-0 ilichokipa Tabora United dhidi ya Simba juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa KMC Complex jiji Dar es Salaam, kimeifanya timu hiyo kuendeleza rekodi mbovu ya ugenini kuanzia msimu uliopita hadi sasa. Kikosi hicho kilichopanda daraja msimu wa 2022-2023 na kucheza Ligi Kuu Bara msimu uliopita kilicheza michezo…

Read More

HISIA ZANGU: Akaunti zetu hazitoshi kwa Mayele tena

MAFARAO wa Misri walikamilisha Ligi Kuu yao wikiendi hii iliyoisha. Watu wa ajabu kidogo. Wakati duniani katika maeneo mbalimbali ligi zinaanza wao ndio wametamatisha ligi yao. Sijui wanatumia mfumo upi ambao unawasiganisha na dunia. Na katika msimu huu ulioisha walikuwa na ugeni wa mchezaji anayeitwa Fiston Mayele. Aliondoka katika ardhi ya Tanzania akiwa shujaa anayetetema….

Read More

Kiboko ya nyavu za EPL ndani ya miaka mitano hawa hapa

LIGI Kuu England imeshuhudia wafungaji mahiri sana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Baadhi ya mastaa walionasa Kiatu cha Dhahabu kwa maana ya kuongoza kwa mabao kwenye ligi ni pamoja na Mohamed Salah, Harry Kane na Erling Haaland huku viungo kama Bruno Fernandes na Kevin De Bruyne wakiongoza kwenye kupika mabao hayo. Kwa miaka mitano…

Read More

PUMZI YA MOTO: Azam Complex imeanzia ilipoishia

 MSIMU wa mashindano wa 2024/25 umeanza nchini Tanzania, kwa mashindano ya ndani na ya nje. Kuanza kwa msimu ni kuanza kwa biashara zote zinazoambatana na mpira, ikiwemo ya viwanja vya kuchezea. Na kama kuna uwanja umeanza kwa kishindo basi ni Azam Complex, uwanja wa nyumbani wa Azam FC, uliopo pale Chamazi. Kwa siku tatu tu,…

Read More