
Jinsi baiskeli ilivyomsaidia kupambana na fisi kwa saa tatu
Sengerema. Bahati Kanfumu, mkazi wa Kijiji cha Kabusuli, Kata ya Nyamatongo, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza ameeleza jinsi alivyonusurika kushambuliwa na kundi la fisi. Akizungumza jana Agosti 11, 2024, amesema wakati akielekea kutafuta mahitaji ya familia asubuhi, alikutana na kundi hilo la fisi linalosadikika kuwaua watu wawili. Amesema alilazimika kushuka kutoka kwenye baiskeli aliyokuwa akiendesha…