
JIWE LA SIKU: Ishu ya Kibu, Mnunka ni yale yale
BAADA ya sekeseke la Kiungo mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis na klabu yake kumalizika kwenye tamasha la Simba Day, kuna sinema nyingine imeubuka kwa Wekundu wa Msimbazi, lakini safari hii ni kwenye timu ya wanawake, Simba Queens. Suala la Kibu lilivyoanza, alisaini mkataba mpya na Simba, Juni mwaka huu uliokuwa na hekaheka nyingi akitaka mkwanja…