
AKILI ZA KIJIWENI: Labda nyie mnamwelewa Kibu Denis
NIMEJARIBU kumwelewa rasta Kibu Denis Prosper ambaye wiki chache zilizopita alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba, maana yake hajaanza hata kuutumikia. Jamaa baada ya kusaini mkataba mpya na msimu wa 2023/2024 kumalizika akaiomba ruhusa klabu yake kuwa anaenda mapumzikoni Marekani ambako pia inaishi. Uongozi wa Simba kiungwana ukamruhusu ukizingatia ni haki na lazima…