Mashujaa yajificha ufukweni Dar | Mwanaspoti

UNAITAFUTA Mashujaa? Basi usiende viwanjani kwani jamaa wako zao ufukweni wakizianza hesabu za kujipanga kwa ajili ya msimu ujao. Wakiwa chini ya kocha mkongwe Salum Mayanga, Mashujaa wamekita kambi yao jijini Dar es Salaam, kujifua kwa mazoezi ya ufukweni. Mashujaa wanafanya tizi wakikimbia mbio tofauti na mazoezi mengine ya fiziki, wakiwa kwenye fukwe za Msasani….

Read More

Staa Nigeria aangua kilio chama likiaga

NAHODHA wa timu ya wachezaji wa ndani ya Nigeria, Junior Nduka ameshindwa kujizuia na kungua kilio baada ya timu yake kutolewa mapema kwenye michuano ya fainali za CHAN kufuatia kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Sudan. Mechi hiyo ya kundi D ilipigwa juzi, Jumanne ya  Agosti 12, 2025 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Dakika chache…

Read More

Dimeji aiponda Nigeria, akikoshwa na Taifa Stars

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Dimeji Lawal, ameonyesha kutoridhishwa kwake na kiwango cha Nigeria (Home-Based Eagles) baada ya kutolewa kwenye michuano ya CHAN huku akiipongeza Taifa Stars ya Tanzania. Nigeria ilikumbana na kipigo kizito cha mabao 4-0 kutoka kwa Sudan katika mechi yao ua pili ya  kundi D, iliyopigwa Jumanne. Kabla ya kipigo…

Read More

Komba, wenzake wafungua kesi kupinga uchaguzi TFF

Wakili Alloyce Komba pamoja na wenzake watatu wamefungua kesi katika Mahakama Kuu wakipinga mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), unaotarajiwa kuhitimishwa Agosti 16, 2025 mjini Tanga. Walioshtakiwa katika kesi hiyo ni Baraza la Michezo la Taifa (BMT), TFF na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakidai kuwa mchakato huo umeendeshwa kinyume cha…

Read More

CHAN 2024: Faini zarindima CAF, Kenya yapewa onyo

KAMATI ya Nidhamu la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imekutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nidhamu katika michuano ya CHAN inayoendelea na kutoa uamuzi kadhaa dhidi ya vyama vya soka vya Zambia, Kenya na Morocco. Katika kikao hicho Shirikisho la Soka Zambia (FAZ) lilipatikana na hatia ya kukiuka Kanuni za vyombo vya habari wakati wa mkutano…

Read More

Morocco haitaki kurudia makosa CHAN 2024

KOCHA wa Morocco, Tarik Sektioui amesema makosa waliyoyafanya kwenye mechi iliyopita dhidi ya Kenya wanayafanyia kazi ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Zambia. Agosti 10, Morocco ilipoteza bao 1-0 dhidi ya Kenya, ikiwa ni mchezo wao wa pili kwenye Kundi A. Mechi ya kwanza walishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Angola, na kuwafanya Waarabu hao…

Read More

Tano tayari, hao Tausi wabayaa

LIGI ya kikapu Dar es Salaam inaendelea kunoga huku timu zilizotinga hatua ya robo fainali zikianza kujulikana na unaambiwa mambo ya kubaniana ‘press’ kwa timu kwa timu, ubora na yale maokoto ya nje ya uwanja yalitawala msimu huu hadi sasa. Ligi ya msimu huu inatajwa ni bora zaidi na hadi sasa tayari timu tano zimeshatinga…

Read More

Yanga yaifuata Rayon, kocha akimwaga nondo

NYOTA 24 wa kikosi cha Yanga wamepaa leo kuifuata Rayon Sports ya Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Romain Folz akiitaja safu ya ushambuliaji. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeiambia Mwanaspoti kuwa kikosi cha Yanga mara baada ya kutua nchini Rwanda kitafikia…

Read More

Jeuri ya pesa, Fei akiamua hatima yake

JEURI ya pesa! Hivyo ndivyo unaweza kusema baada ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye ameshafanya uamuzi wa wapi atakipiga msimu ujao na kinachoelezwa ni kwamba fedha imeongea zaidi. Mchezaji huyo amekuwa akitakiwa na timu mbalimbali za ndani na nje ya nchi ikiwamo Simba na Yanga kwa hapa nchini na pia…

Read More

Kanuni zawabana mashabiki CHAN 2024

MASHABIKI wanaohudhuria mechi mbalimbali za mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 wametakiwa kuzingatia miongozo ya usalama na ulinzi iliyotolewa na Kamati ya Maandalizi (LOC) pamoja na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ili kuepuka adhabu na usumbufu. LOC imeweka bayana mabango, bendera au alama zenye ujumbe wa kisiasa, dini, kibaguzi au…

Read More