
NOELA: Chama wa Kikapu MVP mara 10
UKIMUONA nje ya kazi unaweza kumdharau, lakini ukija kazini kwake utapata stori ya namna anavyosifika kwa uchezaji uwanjani. Noela Uwandameno (22), ambaye ni mchezaji wa Vijana Queens na mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anasimulia namna alivyoingia kwenye mpira wa kikapu na anavyojigawa pia kwenye masomo. “Ni miaka saba sasa tangu nianze kucheza…