Mgunda afichua siri usajili Simba

ALIYEKUWA kaimu kocha mkuu wa Simba, Juma Mgunda amefichua siri za usajili mpya wa klabu hiyo iliyopo kambini Ismailia, Misri na kuupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kufuata ushauri alioutoa wa kutaka kuvunjwa kwa timu hiyo ili isajili wachezaji vijana ambao watajenga timu mpya. Mgunda aliiwezesha Simba kumaliza katika nafasi ya tatu ndani ya Ligi…

Read More

Aliyekuwa kocha Biashara atoa msimamo

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Biashara United ya Mara, Amani Josiah amesema kwa sasa yuko huru baada ya kumaliza mkataba na klabu hiyo huku akikiri kupokea ofa kutoka timu mbalimbali ambazo bado hajazitolea uamuzi akisubiri timu itakayomshawishi kwa ofa nzuri. Josiah aliiongoza Biashara msimu uliopita katika Ligi ya Championship akisaidiana na Edna Lema na Ivo Mapunda,…

Read More

Ufudu ajilipua Mashujaa | Mwanaspoti

BAADA ya kudumu Kagera Sugar kwa miaka minne, Julai 7, mwaka huu kiungo, Ally Nassoro Iddi ‘Ufudu’ alitua Mashujaa FC ya Kigoma akisaini mkataba wa mwaka mmoja, huku akifichua siri ya kujiunga na maafande hao na yuko tayari kupambania namba kikosini hapo. Ufudu ni usajili wa kwanza kutambulishwa na Mashujaa kwenye dirisha hili akifuatiwa na…

Read More

Pamba Jiji yaenda chimbo la wiki tatu

KIKOSI cha Pamba Jiji kitaondoka keshokutwa (Jumapili) jijini hapa kwenda mjini Morogoro kuweka kambi ya takribani wiki tatu kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara chini ya Kocha Mkuu, Goran Kopunovic na msaidizi wake, Salvatory Edward. Wachezaji wa timu hiyo wapya na wale wa zamani wameshaingia kambini tangu Jumatatu kwenye maskani yao eneo la…

Read More

Ukweli kuuzwa kwa Alliance FC ni huu

BAADA ya uwepo wa taarifa za timu ya wavulana ya Alliance FC ya jijini hapa kuuzwa mkoani Arusha, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kutolea ufafanuzi huku ukiwatoa wasiwasi mashabiki wake. Timu hiyo ambayo iliponea chupuchupu kushuka daraja kutoka First League msimu uliopita baada ya kusuasua kwa kile kinachotajwa ni ukata unaoikabili, hivi karibuni zimeibuka…

Read More

Srelio, Crows zaanza na moto

TIMU za kikapu ya Srelio na Crows zimeanza kuzitisha timu zinazoshiriki ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL), baada ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo uliopigwa  kwenye Uwanja wa Don Bosco Youth Centre. Vitisho vya timu hizo vimetokana na timu ya Srelio kuifunga timu ya…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Andabwile, Kagoma nisikilizeni kwa umakini

DIRISHA la usajili lilichangamka sana wiki hii hasa kwa timu mbili vigogo nchini Simba na Yanga ambazo zilitambulisha baadhi ya wachezaji wao na wengine zikawapa ‘Thank You’. Miongoni mwa wachezaji waliotambulishwa ni viungo wawili wakabaji, Yusuf Kagoma na Aziz Andabwile ambao msimu uliopita walikuwa wakiitumikia Singida Fountain Gate. Aziz Andabwile alitambulishwa na Yanga ikionekana ni…

Read More

VETA yaizima B4 ligi ya mkoa Shinyanga

TIMU ya kikapu  ya Veta ilidhihirisha ubora wake baada ya kuifunga timu ya B4 Mwadui kwa pointi 45-39, katika ligi ya kikapu mkoa wa Shinyanga iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mwadui  Kamishina wa ufundi na mashindano wa mkoa huo, George Simba aliliambia Mwanaspoti kwamba, ameridhishwa na ushindani ulioonyeshwa na timu zote mbili katika mchezo huo uliokuwa…

Read More

NIONAVYO: Kombe la Kagame, Walioitwa hawaitiki

MICHUANO ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inaendelea jijini Dar es Salaam. Hii ni moja ya michuano ya muda mrefu ya klabu Afrika. Awali yalijulikana kama Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati na baadae mwaka 2002, yaliitwa Kombe la Kagame baada ya kudhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye ni…

Read More

DB Troncatti yazidi kutesa BDL

TIMU ya DB Troncatti inaendelea kutesa katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL) upande wa  wanawake, ikionyesha ubabe kwa kuifunga timu DB Lioness kwa pointi 72-55. Katika mchezo huo, DB Troncatti iliongoza katika robo ya kwanza  kwa pointi 19-12, 17-12, 22-16 na 14-15. DB Troncatti  ilimaliza mzunguko wa kwanza kwa kutopoteza mechi…

Read More