Beki la Ivory Coast lakubali miwili Simba

HATIMAYE Wekundu wa Msimbazi, Simba wamefikia makubaliano na Racing Club Abidjan ya Ivory Coast kwa ajili ya kupata huduma ya beki wa kati, Chamou Karaboue, 24, huku Ahoua Jean Charles akitajwa kuwa nyuma ya dili hilo. Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa Karaboue amekubali ofa ya kusaini Simba  mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza…

Read More

Wachezaji vijana waonyeshe upekee 2024/2025

Ni Julai ambapo baadhi ya timu zimeanza rasmi kambi za maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/2025. Kwa wale wachezaji ambao timu zao bado hazijaanza kambi za maandalizi ya msimu, kwa sasa wapo wanamalizia likizo zao ingawa hapana shaka nao muda sio mrefu wataenda kujiandaa kama ambao wenzao wameanza sasa. Kuanza kwa maandalizi ya…

Read More

Anguti Luis atua Coastal Union, kukiwasha KAGAME CUP

Beki Anguti Luis atakuwa sehemu ya kikosi cha Coastal Union msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Beki huyo kutoka nchini Uganda anajiunga na Coastal Union akitokea KCCA ya nchini kwao, na tayari ametambulishwa na klabu hiyo ya jijini Tanga. Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii…

Read More

Mrithi wa Inonga Simba yupo hapa!

SIMBA inaendelea kusajili majembe mapya, ikiwamo jana kumtambulisha Abdulrazak Hamza kutoka Cape Town City ya Afrika Kusini sambamba na mrithi wa Clatous Chama, nyota kutoka Ivory Coast, Ahoua Jean Charles na sasa inapambana kushusha beki wa kuziba nafasi ya Henock Inonga aliyetua FAR Rabat ya Morocco. Mezani kwa mabosi wa Simba ina majina manne ya…

Read More

Baleke, Yanga jambo lao lipo hivi

HIZI huenda zikawa taarifa za kushtukiza kwa mashabiki wa soka nchini, kwamba baada ya Yanga kumbeba Clatous Chama kutoka Simba na Prince Dube aliyekuwa Azam, sasa inafanya mipango ya kumshusha kikosini, Jean Baleke aliyewahi kuwika na Wekundu wa Msimbazi hata miezi sita tu iliyopita. Ndio, hivi unavyosoma Mwanaspoti ni kwamba kuna uwezekano wa asilimia 99…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Mamelodi wameonyesha ukubwa kwa Mokwena

HAIKUONEKANA kama maisha yangeenda kasi kwa kocha wa mpira Rhulani Mokwena baada ya mafanikio aliyoipa Mamelodi Sundowns. Miezi michache iliyopita aliongeza mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa miaka minne zaidi kwa kile ambacho kilitafsiriwa na wengi kwamba kuna imani ya uongozi kwa kocha huyo. Mataji matatu ambayo aliiongoza Mamelodi Sundowns kunyakua msimu uliomalizika yalionekana yangekuwa…

Read More

Viwanja vinne kutumika Ligi ya kikapu Mara

MASHINDANO ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mara yanatarajiwa kuanza Julai 7 mwaka huu, huku katibu mkuu wa chama cha mchezo huo cha mkoa huo, Koffison Pius akitangaza viwanja vinne vitakavyotumika kwa ngarambe hiyo ya kusaka bingwa. Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Mara, Pius alitaja viwanja hivyo ni Musoma Matumaini, Chuo cha…

Read More