Msimu ujao labda msilete timu

VIGOGO vya soka nchini, Simba, Yanga na Azam FC vipo bize kushusha na kutambulisha mashine mpya kwa ajili ya msimu utakaoanza Agosti, kiasi huko mtaani na kwenye mitandao ya kijamii mashabiki na wapenzi wanatambiana. Wale wa Yanga wanawatania Simba wakiwatisha eti labda wasipeleke timu uwanjani kwani badala ya kupigwa 7-2 kama msimu uliopita, safari hii…

Read More

Tabora Utd yamvutia waya kocha Baraza

MABOSI wa Tabora United wameanza mazungumzo na aliyekuwa kocha mkuu wa Dodoma Jiji, Francis Baraza kwa ajili ya msimu ujao. Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zinasema viongozi wamefungua mazungumzo na Baraza ili kukabidhiwa timu ikiwa ni muda mfupi tangu alipotemwa Dodoma Jiji na nafasi yake kuchukuliwa na Mecky Maxime. “Ni kweli mazungumzo hayo yapo…

Read More

Aucho amchambua Mukwala. Ngoma atamba kubeba ubingwa

MABOSI wa Simba wanaendelea kushusha mashine mpya kwa ajili ya kutengeneza kikosi cha msimu ujao, lakini kiungo nyota wa timu hiyo, Fabrice Ngoma ameshindwa kujizuia akisema kwa aina ya wachezaji wanaotua Msimbazi anaona kabisa msimu ujao Wekundu hao wakirejesha mataji waliyoyapoteza kwa Yanga. Ngoma amesema kinachompa jeuri ya kuitabiria Simba kubeba ndoo ilizozitema kwa Yanga…

Read More

Yanga yaanza na ‘Thank You’ mbili kimyakimya

YANGA imeanza kutoa ‘thank you’ kimyakimya, ambapo imeshawaaga nyota wawili akiwemo kipa, Metacha Mnata na kiungo mmoja, Zawadi Mauya. Yanga imemuaga aliyekuwa kipa wa timu, Metacha Mnata ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi cha msimu ujao wa 2024-25 baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja na nusu. Kipa huyo alijiunga na Yanga, Januari 2023 akitokea Singida Fountain…

Read More

Kocha mpya Simba huyu hapa, kutua Ijumaa na fulu mziki

UONGOZI wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili aliyekuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca, Fadlu David anayeelezwa atatua nchini Ijumaa sambamba na wasaidizi wake. Kocha huyo ambaye amethibitisha ujio wake Tanzania baada ya kutumia ukurasa wake mtandao wa kijamii ‘Instagram’ kuwaaga viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu aliyokuwa akiifundisha. “Ulikuwa ni wakati mzuri,…

Read More

Lusajo atua Dodoma Jiji | Mwanaspoti

KLABU ya Dodoma Jiji imekamilisha uhamisho wa aliyekuwa mshambuliaji wa Mashujaa, Reliants Lusajo kwa mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwingine baada ya kuvutiwa na uwezo aliouonyesha msimu uliopita. Nyota huyo aliyeanza msimu na Namungo kisha Januari akajiunga na Mashujaa kwa miezi sita, amejiunga na kikosi hicho baada ya kuvutiwa na…

Read More

Stars mtegoni Afcon 2025 | Mwanaspoti

WAKATI droo ya kuwania Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 zitakazopigwa Morocco ikifanyika leo, timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ipo katika mtego wa kuangukia kundi gumu au mchekea kwenye droo hiyo ya upangajwaji wa makundi itakayochezeshwa leo Afrika Kusini. Katika droo hiyo ambayo itachezeshwa jijini Johannesburg kuanzia saa 9:30 alasiri kwa muda…

Read More