
CCM yakusanya zaidi ya Sh86 bilioni chini ya saa 24
Dar es Salaam. Ndani ya saa 24, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimekusanya zaidi ya Sh86 bilioni katika harambee iliyoanzishwa ya kuchangia shughuli za kampeni za urais na ujenzi wa chama hicho. Kati ya fedha hizo, zaidi ya Sh56.3 bilioni zimelipwa papohapo, huku zaidi ya Sh30.2 bilioni ni ahadi zinazotarajiwa kulipwa na wadau, makada na washabiki…