Mastaa Umitashumta kuitwa Stars | Mwanaspoti

WAKATI Shirikisho la Soka nchini (TFF) likiwa limeshapokea barua ya kustaafu kuitumikia Taifa Stars ya nahodha, Mbwana Samatta, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro ametaja mikakati ya kupata warithi wa wachezaji waliopo na mastaa wa baadae. Ndumbaro ambaye alikiri kupokea barua ya Samatta, alisema wizara imeshatoa maelekezo kwa vyama vyote vya michezo…

Read More

Ibenge aingilia ishu ya Chama

KOCHA maarufu kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kaskazini anayeikochi Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge amefafanua jambo kuhusiana na staa mpya wa Yanga, Clatous Chama. Mzambia huyo alijiunga na Yanga juzi Jumatatu akitokea Simba aliyomaliza nayo mkataba baada ya kuitumikia kwa mafanikio ikiwemo kuipeleka kwenye robo fainali za mashindano ya klabu Afrika mara…

Read More

Simba mpyaa Mnahesabu hukoo.. | Mwanaspoti

TAYARI Joshua Mutale kiraka wa Zambia ameshatambulishwa rasmi Msimbazi. Jana mchana ilikuwa zamu ya Steven Mukwala, staa wa Uganda. Lakini sasa unaambiwa Simba imetuma tiketi mbili za ndege katika mataifa mawili tofauti ili kuwashusha nchini wachezaji wawili matata akiwemo mrithi wa Clatous Chama aliyetangazwa kujiunga na Yanga, juzi. Kati ya tiketi hizo moja imeenda Kinshasa,…

Read More

Azam waipa Simba bei ya Fei Toto

SIMBA na Mamelodi Sundowns zimeulizia uwezekano wa kumsainisha mkataba staa wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ lakini zikaambiwa hauzwi. Fei Toto ambaye alitua Azam FC akitokea Yanga, alisaini mkataba wa miaka mitatu na tayari ameutumikia kwa msimu mmoja akiisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika Ligi…

Read More

Majiha katika nyakati za kudhihirisha umwamba wake

JULAI 20, mwaka huu bondia namba moja nchini ‘Tanzania One’ Fadhili Majiha maarufu Kiepe Nyani atapanda ulingoni kutetea Mkanda wa ubingwa wa Baraza la Ngumi Duniani kwa Tawi la Afrika ‘WBC Afrika’ ambalo limepangwa kufanyika katika Jiji la Mbeya. Majiha atapanda ulingoni kwenye pambano hilo dhidi ya Sabelo Ngebinyana wa Afrika Kusini katika pambano litakalokuwa…

Read More

Lebron amsubiri Klay Killers Lakers

DIRISHA la usajili kwa wachezaji huru (free agents) lipo wazi kwa sasa kwenye Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), ambapo wachezaji wanatoka timu moja na kwenda nyingine na hata zaidi ya timu moja kupitia mabadilishano. Usajili unaosubiriwa zaidi  ni ule wa Klay Thompson ‘Killer’ kujiunga na Los Angeles Lakers ya LeBron James ambaye inaelezwa kuwa yupo…

Read More