
Norris shubiri mpya kwa Verstappen
MBIO zilizopita za nchini Austria zilisisimua vilivyo wapenzi wa mashindano ya magari duniani (Formula 1) kutokana na kilichotokea kati ya madereva Max Verstappen na Lando Norris. Wakiwa wanafukuzana kwenye mbio sita za nyuma, wawili hao waliiingia kwenye vita ya kuwania ushindi wa mbio za Austria, na vita baina yao ilikwenda hadi mwishoni kabisa ilipobaki mizunguko…