KenGold mguu sawa Ligi Kuu

MKURUGENZI Mtendaji wa KenGold, Kenneth Mwakyusa Mwambungu amesema kwa sasa wanaendelea na zoezi la kuboresha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, huku akiweka wazi watazingatia matakwa yote kutoka kwa benchi la ufundi. Akizungumza na Mwanaspoti, Mwambungu alisema licha ya ukimya uliopo ila wanaendelea na mikakati ya kuisuka timu hiyo huku…

Read More

Dabo hataki kurudia makosa msimu

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amefunguka hataki kurudia makosa ya msimu uliopita katika michuano ya kimataifa na kusema ndio sababu iliyomfanya awaite mapema kambini mastaa wa timu hiyo ili kutengeneza muunganiko baada ya sajili mpya na kuiweka timu freshi kabla ya kuliamsha 2024-2025. Msimu uliopita Azam licha ya kumaliza nafasi ya pili katika…

Read More

Zawadi Mauya afunguka yaliyojificha Yanga

KIUNGO aliyemaliza mkataba Yanga, Zawadi Mauya ameizungumzia misimu minne ndani ya kikosi hicho jinsi ilivyompa upana wa kufanya kazi yake kwa weledi, licha ya kushindwa kuanika dili la kutua Singida Black Stars (zamani Ihefu) inayodaiwa kumpa mkataba wa miaka miwili. Mauya alijiunga na Yanga, Julai Mosi 2020 ambapo msimu ulioisha alimaliza mkataba na Mwanaspoti limepata…

Read More

TETESI ZA USAJILI BONGO: Nahimana anajiandaa kusepa Namungo

KIPA wa kimataifa wa Burundi, Jonathan Nahimana anayeidakia Namungo huenda msimu ujao asiwe sehemu ya kikosi hicho baada ya kukichezea kwa miaka minne. Inaelezwa Namungo haina mpango wa kumwongeza mkataba Nahimana ambaye aliichezea mechi 34 na mwenyewe ameanza kufikiria maisha mapya nje ya timu hiyo ya Kusini mwa Tanzania. Namungo inatajwa kumalizana na kipa wa…

Read More

MTU WA MPIRA: Hata Chama mwenyewe anawashangaa Simba

KUNA vitu vingine vinaendelea nchini vinashangaza sana. Ni kama hili sakata la usajili wa Clatous Chama. Ni jambo la kushangaza. Huko mitandaoni kumechafuka. Huyu anasema Chama ni wa Simba mwingine anakuja anasema ni wa Yanga. Ni mkanganyiko mkubwa. Kwanini, subiri nitakwambia. Chama alikuwa mchezaji wa Simba hadi msimu unamalizika. Amecheza Simba tangu 2018 ukiacha miezi…

Read More

Kocha Nabi afunguka walivyomalizana na Inonga

KOCHA wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema wala sio ishu mpya kwa beki Mkongomani kusajiliwa FAR Rabat ya Morocco, kwani jamaa alishamalizana nao kitambo kisha akasema atapiga kazi ya maana. Inonga inaelezwa amesaini miaka mitatu ya kuichezea timu hiyo aliyokuwa akiinoa Nabi na kuifanya imalize nafasi ya pili, ikiukosa kiduchu ubingwa mbele ya Raja…

Read More

Hatima ya Guede yaibua makundi mawili Yanga

KUMEZUKA makundi mawili ndani ya Yanga juu ya hatima ya mshambuliaji Joseph Guede, huku kila moja likiwa na hoja zake kwamba jamaa abaki au apewe ‘thank you’. Yanga inataka kuachana na washambuliaji wake wawili Kennedy Musonda na Guede, kisha zitafutwe mashine zingine ikiona kama jamaa hawajafanya makubwa ingawa wote wameitumikia timu hiyo kwa nyakati tofauti….

Read More

Tshabalala apewa mtihami Simba, aletewa chuma

WAKATI Simba ikiendelea kuweka mambo sawa katika dirisha hili la usajili linaloendelea, imeshusha chuma ambacho ujio wake unatajwa kuwa unakwenda kuleta changamoto kwa nahodha msaidizi wa timu hiyo, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ katika eneo analocheza la beki wa kushoto. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni baada ya miaka zaidi ya sita kupita ikimshuhudia Tshabalala akitamba atakavyo katika…

Read More

Ajibu aikacha Coastal akimbilia jeshini

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba, Yanga, Azam na Singida FG aliyekuwa akikipiga Coastal Union, Ibrahim Ajibu amesaini mkataba wa miaka miwili na maafande wa JKT Tanzania. Ajibu aliyeichezea Coastal kwa mafanikio akiwa nahodha akisaidiana na wenzake waliifanya timu hiyo imalize ya nne katika Ligi Kuu Bara hivi karibuni na kukata tiketi ya Kombe la…

Read More