
NYUMA YA PAZIA: Hakimi alivyokwepa kutoka jasho Ujerumani akakimbilia Arusha
NIMEMUONA Achraf Hakimi Mouh akizurura pale Arusha. Kuzurura? Hapana! Sio neno zuri hasa ukizingatia kwamba ametoa kiasi cha Sh1 bilioni kusaidia watoto wenye uhitaji katika kituo kimoja cha watoto wa aina hiyo pale Arusha. Jana alitua Zanzibar. Hakimi amenikumbusha mbali. Amenikumbusha mambo mengi. Kwanza amenikumbusha pesa. Ndio, pesa ni sabuni ya roho. Pesa ni kila…